BEKI 'KISIKI' WA VILLAREAL AKARIBIA KUTUA ARSENAL


Kocha wa Arsenal  Arsene Wenger amesema klabu yake iko katika mazungumzo na Villarreal kuhusu kumsajili beki Gabriel Paulista.


Arsenal wana nafasi kubwa kupata saini ya beki huyo raia wa Brazil mwenye miaka 24 tayari wakiwa wamemsaini beki mwenye miaka 17 Krystian Bielik toka Legia Warsaw ya Poland kwa ada ya uhamisho  £2.4m wiki hii ambaye Wenger anaamini anaweza kucheza kama kiungo.

Wenger anaamini kuwa kuna uwezekano mkubwa wakampata Paulista ambaye klabu yake inataka paundi milioni 15 kumwachia na Wenger anasema wako tayari kulipa pesa ambayo ni sahihi kwa mchezaji mzuri.

Kocha Arsene Wenger pia amezungumzia hali ya majeruhi katika timu na kutanabaisha kuwa Hector Bellerin anaweza kucheza katika mechi ya Jumamosi hii ya kombe la FA dhidi ya Brighton ila Alex Oxlade-Chamberlain mwenye tatizo la misuli ya paja bado hakuna uhakika wa kurudi uwanjani.

Kuhusu Danny Welbeck Bosi huyo wa Arsenal amesema Welbeck atahitaji mechi mbili au Tatu kurudi katika hali yake ya awali

No comments

Powered by Blogger.