WAPENDASOKA DAY KAZI IMEIVA, WASHIRIKI WAANZA KUKAKABIDHIWA T-SHIRT ZAO NCHI NZIMA
![]() | |
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Wapendasoka Day, Bab Chicharito akimkabidhi T-shirt mwanadada Cataleya Dot Fortue mapema mwezi huu jijini Dar es Salaam. |
Ile siku inayosubiriwa kwa hamu kubwa na familia kubwa ya wapendasoka nchini Tanzania, inazidi kusogea, huku maandalizi yakiwa yamepamba moto. Mapema mwezi huu, washiriki wa sikukuu hiyo pendwa wamekuwa wakikabidhiwa T-shirt maalumu wa ajili ya siku hiyo ambayo wapendasoka huitumia kutoa misaada kwa watoto yatima wenye uhitaji.
Sikukuu hiyo ambayo huadhimishwa kila tarehe 1 Januari, imekua na mvuto wa aina yake mwaka huu kutokana na kuambatana na maadhimisho ya miaka mitano ya familia hiyo ambayo ilianzishwa miaka mitano iliyopita, huku siku hiyo ikiwa inaadhimishwa kwa mwaka wa tatu sasa.
![]() | ||||
Bab Chicharito (kushoto) akimkabidhi shabiki machachari wa Arsenal, Arsenalized Derick T-shirt yake mwishoni mwa juma lililopita huko jijini Mwanza |
Akizungumza na mtandao huu, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sikukuu hiyo Bab Chicharito alisema, "Tunataka kufanya kitu kitakachoonesha hatua moja zaidi kutoka Wapendasoka Day ya mwaka uliopita.
Mwisho wa wiki hii tutatangaza kituo cha watoto yatima tutakachokitembelea. Kwa sasa naweza kusema maandalizi yamepamba moto na bado nawaomba watu waendelee kutoa michango kwa ajili ya kusaidia watoto yatima"
Alisema Bab, aidha aliongeza kwamba safari yake ya Mwanza ilikua ya mafanikio sana, "Nilienda Mwanza kwa shughuli zangu binafsi, lakini niliitumia pia fursa hiyo kukutana na Wapendasoka walioko kule na kuwakabidhi T-shirt zao, lakini pia kuendelea kukusanya michango na nashukuru kwa yote"
![]() |
Mpendasoka mwingine kutoka Mwanza Alex Sanga nae akikabidhiwa T-shirt yake |
Kurugenzi ya mawasiliano ya Wapendasoka inatarajia kutangaza kituo cha watoto yatima kitakachotembelewa mwaka huu, lakini mtandao huu unaelewa kwamba kituo kicho kipo mjini Bagamoyo na taratibu za mwisho zinafanyika ili kukamilisha hilo.
![]() |
Adrian Chibo nae ni mmoja kati ya waliopokea T-shirt zao jijini Dar es Salaam |
Hayo yalisemwa na Richard Leonce Chardboy ambae ni msemaji wa kurugenzi ya mawasiliano ya Wapendasoka ambayo ndio inayoendesha mtandao huu.
![]() |
Mpendasoka huyu hakutaka kusubiri, alipigilia uzi wake palepale |
Lakini pia Chardboy hakusita kuwakumbushia Watanzania wote wenye nia njema kuendelea kutoa michango yao kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima. "unajua mahitaji ni makubwa sana, watoto wanahitaji sare za shule, vifaa kama daftari, kalamu nk.
chakula, mavazi. hivyo ni wazi kwamba sisi peke yetu hatuwezi, ndio maana bado nawasihi Watanzania wote wenye mapenzi mema watuunge mkono ili tuwasaidie masikini wenzetu. ni jukumu letu sote"
![]() |
T-shirt zikiwa tayari kwa ajili ya Wapendasoka Day |
Namba za simu za Tigo Pesa na M pesa kwa ajili ya michango hiyo zinapatikana katika blog hii, juu kabisa ila kwa mawasiliano zaidi unaweza kupiga namba 0715 127272 (Edo) 0717 685055 (Bab Chico) kupata mchakato mzima unavyoendelea
![]() |
Mwenyekiti Bab Chicharito akirejea jijini Dar es Salaam. |
No comments