INASIKITISHA HALI YA ARSENAL NA ARSENE WENGER INAOGOPESHA NDANI NA NJE YA UWANJA.
Jumamosi tarehe 6 desemba 2014,Mida ya saa 12 na nusu jioni kuelekea sa moja jioni kasoro, saa za Uingereza,Arsene Wenger pamoja na wachezaji wa Arsenal walikua wakielekea kupanda train kwenye kituo cha Brittania train Station.
Ilikua ni baada ya kumalizika kwa mechi ya Stoke city na Arsenal iliyoisha kwa ushindi wa Stoke city kushinda 3-2.
Ghafla kundi kubwa la mashabiki wa Arsenal lilitokea karibia na Arsene Wenger, lilianza kumzomea, kumdhihaki na kumtukana.
Mshabiki wa mmoja mwenye hasira alivuka mipaka na kudiriki kusema..
" Fuck off...leave my club"
(Video ipo youtube itafute)
Inavoonekana tukio ili lilipangwa, ndo mana alierekodi video hii alikua "standby". Nia nafikiri ilikua ni kuonesha ulimwengu, na wamefanikiwa kwa sababu dunia ni kijiji kwa sasa.
Well, me siandiki makala mara nyingi, lakini kitu kikinigusa, nikipata muda naandika. Haya ni maoni yangu binafsi, hayawezi kufanana na maoni ya wengine. Lakini kitendo hichi kinasikitisha na kinaashiria hali mbaya sana itakayokuja kutokea kama mambo yatabaki kua hivi hivi.
Its very sad, kuona Kocha maarufu na mwenye mafanikio makubwa kwenye historia ya club yenye hadhi kama ya Arsenal amefikia katika hali kama hii. Inasikitisha sana, kuona mmoja ya makocha wenye kazi nzuri kabisa kwenye biashara ya soka, anapata dhihaka kama hii.
Inasikitisha kwa kocha aliyeipa identity/utambulisho Arsenal, aliyeisaidia kuieka kwenye ramani ya soka Ulaya, alieipa heshima kubwa duniani, alieisaidia kujenga uwanja wa kisasa kabisa duniani, amefikia kwenye hali mbaya kama hii.
Naam, usinielewe vibaya, sio kwamba namtetea mzee Wenger, au nataka aendelee kubaki klabuni, But nasikitika kuona kwa yote aliyoyafanya huko nyuma, yanaishia hewani, na mwisho wake unakua wa aibu namna hii.
Kuzomea ni kitu cha kawaida kwenye mpira, mkifungwa mashabiki wanazomea, substution mbaya ikifanyika, rafu mbaya, uamuzi m'mbaya wa waamuzi n.k yote huwa inapokelewa na kuzomea.
Lakini zomea ya hii inayotoka kwa Arsenal, ni tofauti. Mashabiki wamechoka, wamevumilia, wamechoka. Sidhani kama kuna mashabiki au management/uongizi wavumilivu kama hawa wa Arsenal, Lakini huku kuzomea, na matusi juu, kuna ashiria, mambo yanaenda kombo.
Wiki moja iliyopita kwenye uwanja wa Westbromwich Albion, japokua Arsenal ilipata ushindi na ilicheza vizuri, mashabiki baada ya mechi walionekana wakishika bango lilioandikwa
"ARSENE, THANKS FOR THE MEMORIES BUT ITS TIME TO SAY GOODBYE"
Imani ya mashabiki kwa Arsenal Wenger imekwisha, na hata wachezaji nafikiri wanapokea maelekezo kwa Kocha wao lakini wanayatimiza kwa mechi 2 au 3, then wanayasahau au kuyapuuzia.
Ok, Wenger anaeza kusema kua msimu huu Arsenal amekua na bahati mbaya ya kupata majeruhi, especially kwenye safu ya ulinzi, lakini Wenger anajua historia ya hii timu, hakufanya vizuri kipindi cha usajili. Naweza kusema vitu vingine kama falsafa, misimamo na kiburi chake kinamtokea puani Mzee Wenger.
Kwa miaka 10, Arsenal imeshindwa kushindana na Chelsea, Manchester united na ujio wa Manchester City umeiangusha Arsenal kabisa.
Muhusika mkuu wa majanga haya anaonekana ni kocha.
Na hii inasababishwa na kufeli kwenye mipango ya usajili, na kufanya makosa yale yale, miaka nenda rudi. Nafikiri hii ndo sababu, mashabiki wamemgeuka kocha Arsene Wenger. Anaonekana ni mtu asiejifunza na makosa.
Ni aibu kwa klabu kama Arsenal kushindwa kununua beki bora, na kuanza kuchezesha wachezaji wenye uzoefu mdogo, au kucheza wachezaji nje ya sehemu zao asili za kucheza.
Ni aibu kwa club kama Arsenal kufungwa 3-0 na klabu iliyokua nafasi ya 13, Stoke city, kwa style ile. Sishangai kuona hasira za mashabiki, hawajazoea hali hii.
Alivyokuja Arsene Wenger mwaka 1996, wote Manchester united and Arsenal walikua na vikombe 10 vya ubingwa wa Uingereza.
Sasa hivi Arsenal ina vikombe 13, na manchester united inavyo 20.
Ok, mzee anasifiwa kwa kuipeleka Arsenal Uefa kila msimu. Lakini iyo si mila na desturi za klabu kama Arsenal, mila yake ni vikombe.
Hizo ni ndoto za klabu kama, Everton, Tottenham, westham n.k...
Lakini kwa arsenal, ni kawaida, hii ni timu yenye jina na heshima kubwa Ulaya.
Nini kifanyike sasa, well i dont know. Akiondoka Arsene Wenger leo hii, Arsenal itamaliza ligi nafasi ya 15. Nafikiri Uongozi wa Arsenal wangeanza kupanga maisha bila ya huyu mzee mapema kabla ya mwezi May,mwaka 2016
Maoni yangu, Arsene Wenger hapaswi kufukuzwa kama mbwa, kwa yote aliyoifanyia Arsenal anastahili kuondoka kwa heshima, ndo maana unaona hata Uongozi bado upo kimya.
Ni wasiwasi wangu pia, viongozi wa Arsenal, wana uwezo mdogo wa mambo ya mpira( Mr Chips na Mr Kroenke). Wanaweza chagua mrithi kituko. Naamini hiyo kazi ya kuchagua Mrithi wamemwachia mzee Wenger aifanye.
Arsene Wenger anaweza kuondoka na kujengewa sanamu ya heshima(na anastahili)
Lakini je atajengewa sanamu kama ya Mkongwe maarufu wa liverpool, Billy Shakly??
Chini ya sanamu ya Billy Shakly yameandikwa maneno haya...
"HE MADE PEOPLE HAPPY"
Does Arsene Wenger, actually make people Happy?? I doubt. Sanamu yake itaandikwaje? He made fans boo him, or he created the invisible arsenal.
Wenger bado ana mchango muhimu kwa arsenal, kwa mfano, kumnunua na kumshawishi sanches ajiunge na Arsenal badala ya liverpool. That was smart.
Lakini bado anaweza kubadilisha hali ilioko saivi, yote hiyo iko mikononi mwake! Kujenga na kubomoa, nyundo na cement/matofali anayo yeye Mzee wenger.
Fränk Victör.
Wapendasoka blog.
No comments