WAPENDA SOKA KUTEMBELEA WATOTO YATIMA JANUARY MOSI
... Jana kupitia kundi la WAPENDA SOKA DAY 1 JAN 2015 katika mtandao wa Whatsapp tulikubaliana kupitisha chaguo moja la muundo wa tshirts mpya za Wapenda Soka ambazo zitazinduliwa rasmi siku ya Wapenda Soka tarehe 1, Januari 2015.
WAPENDA SOKA DAY NI NINI?
Hii ni siku maalumu ya WAPENDA SOKA ambayo tulikubaliana iwe kila mwanzoni mwa mwezi Januari yani tarehe 1.
Ni mwaka wa tatu sasa tunatarajia kuadhimisha siku hii na Lengo kuu la siku hii kama tulivyokubaliana awali ni kujitolea kwaajili ya watu wenye uhitaji (Yatima na waishio katika mazingira magumu)
Hivyo basi tulikubaliana kila Mpenda Soka atoe mchango wake ambao tutakusanya na kufanikisha jambo hili la shukrani kwa Mungu kwa kumaliza mwaka na kuanza mwaka mpya.
Na kwa mwaka huu ilikubaliwa kila atakayeguswa atoe si chini ya 20,000 (Elfu Ishirini) ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi wakati ambao tukiazimisha mwaka wa 5 wa uhai wa kundi la Wapenda Soka (Kandanda)
KUHUSU T-SHITS
Ili kupamba siku hiyo Wapenda Soka tumekubaliana kuwa na fulana maalumu ambazo zitatutambulisha sisi ni nani na kama nilivyosema hapo awali tulipitisha moja kati ya logo ambazo Wapenda Soka walipitisha ambazo zitakua katika fulana hizo.
UPATIKANAJI WA T-SHIRTS
Katika picha tumeweka sample za Tshirts hizo ambazo kamati maalumu ya siku ya Wapenda Soka ilipendekeza zitauzwa kama ifuatavyo :-
1. TZS 10,000 - kwa wale tu ambao watashiriki nasi kufanikisha shughuli nzima ya siku hiyo kwa michango yao.
2. TZS 15,000 - Kwa ambao watahitaji tshirts hizo nje ya Washiriki wa siku ya Wapenda Soka
Upatikanaji wa tshirts hizi ni kwa kila mpenda Soka kwa walio Dar tutakua na huduma ya kukufikishia bure pale ulipo ila kwa wale wa mikoani itabidi utume na pesa ya kukufikishia hapo ulipo na tumefanya hivi kwakua bado kundi letu halijajiimarisha kifedha.
WITO WETU
Kwa niaba ya kamati ya Wapenda Soka Day tunahimiza watu kumalizia michango yao waliyoahidi na kama hukuahidi au ulikua hujui hujachelewa ni wakati wako sasa kutoa ahadi yako au mchango wako ili kufanikisha jambo hili.
Tunaendelea kuwashukuru kwa moyo wenu wa kujitolea kufanikisha jambo hili Muhimu kwetu na kwa Yatima ambao wanategemea misaada yetu ikiwa ni njia mojawapo pia ya kumshukuru Mungu ( How Many People you help is how you measure the Success)
SAMBAZA UPENDO KWA KUSAIDIA WENGINE
ASANTENI
Kwa mawasiliano
.... Imetolewa na Kamati ya Wapenda Soka Day na kurugenzi ya mawasiliano Wapenda Soka (Kandanda)
Kwa mawasiliano
0717 685 055
0715 127272
0766 399 341
Kwa mawasiliano
0717 685 055
0715 127272
0766 399 341



No comments