LUIS VAN GAAL ASHANGAZWA YEYE KUWANIA KOCHA BORA WA MWAKA WA FIFA


Kocha wa MANCHESTER UNITED Luis Van Gaal ambaye amerithi mikoba ya David Moyes ameshangazwa na yeye kuwemo katika list ya makocha wanaowania taji la kocha bora wa mwaka wa dunia ambalo hutolewa sambamba na tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Balon d'or.



Luis Van Gaal anaamini yeye sio kocha bora kwa mwaka huu kwani Manchester United imekua ikisuasua katika ligi kuu pamoja na kutolewa mapema katika kombe la Capital One.

Manchester United imeshinda mechi nne tu msimu huu kati ya mechi 11 za Ligi Chini ya Luis Van Gaal ikikamata nafasi ya 7 hivi sasa na kocha huyo anaamini wapo makocha wengi ambao wangestahili tuzo hiyo kwa mwaka huu lakini kumweka yeye pale hajui wametumia vigezo gani.

Van Gaal anawania tuzo hiyo pamoja na makocha Carlo Ancellot wa Real Madrid, Diego Simeone wa mabingwa wa La liga Atletico Madrid, Jose Mourinho wa Chelsea pamoja na Pep Guadiola wa Bayern Munich.

Tuzo hizo pamoja na zile za mchezaji bora wa dunia zitatolewa Januari 12 mwaka 2015.

No comments

Powered by Blogger.