SIMBA YASAKA USHINDI WA KWANZA LEO TAIFA
Baada ya kutoka sare katika michezo yote 6 iliyopita Simba SC leo wataingia tena uwanjani wakiwa na lengo moja tu la kusaka ushindi wao wa kwanza tangu kuanza kwa ligi kuu soka Tanzania Bara
Simba Inaingia katika uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam kuwaalika maafande wa Ruvu Shooting kutoka Pwani katika mwendelezo wa Ligi kuu mzunguko wa Kwanza.
Simba imeshacheza michezo 6 mpaka sasa ikiwa katika nafasi ya 12 ikiwa haijashinda wala kufungwa mchezo wowote wakati michezo yote hiyo ikiisha kwa sare huku ikiwa imeshafunga magoli 6 na kufungwa magoli 6.
Ruvu Shooting kwa upande wao wameshacheza michezo 6 wakishika nafasi ya 10 ikishinda michezo miwili ikitoka sare mchezo mmoja na kufungwa michezo mitatu. Huku ikiwa imeshafunga magoli manne na kufungwa magoli 7.
Mchezo uliopita Simba ikisafiri mpaka Morogoro ililazimishwa sare na Mtibwa Sugar ya bao 1-1 mchezo ambao kama kawaida Simba walitangulia kufunga bao la kwanza kupitia kwa nahodha George Owino kabla ya Musa Mgosi kusawazisha.
Mchezo mwingine leo utakua kati ya JKT Ruvu watakaoialika Ndanda FC kutoka Mtwara mchezo utakaopigwa katika dimba la Chamazi.
-----------------------------------------

No comments