RONALDO NA MESSI USO KWA USO OLD TRAFFORD MECHI YA KIRAFIKI




Wachezaji Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ambao huwezi kuzungumzia soka kwasasa bila kuwataja watakutana mwezi huu tarehe 18 katika mchezo kimataifa wa kirafiki baina ya Argentina na Ureno nchi ambazo jukumu la unahodha wamekabidhiwa wakali hao mchezo ambapo utapigwa katika dimba la Old Trafford jijini Manchester Jumanne Ijayo kuanzia majira ya Saa 4 kasorobo usiku kwa saa za Afrika Mashariki.



Kuna taarifa zimezagaa duniani leo kuwa Ronaldo alimtukana Messi na Ronaldo hakusita kukanusha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa facebook akisema kuwa hajawahi kumtukana Messi na anamheshimu kama anavyowaheshimu wachezaji wengine.

Kivutio katika mchezo huo itakua kurudi kwa Carlos Tevez katika timu ya Taifa baada ya kusota nje ya kikosi cha Argentina kwa miaka mitatu lakini pia itatoa fursa kwa wachezaji waliowika wakiwa katika kikosi cha Manchester United kurudi tena katika dimba la Old Trafford.

Cristiano Ronaldo, Carlos Tevez na Luis Nani watakumbushia enzi zao walipocheza kwa mafanikio katika kikosi cha Man United hasa mwaka 2008 walipochukua ubingwa wa Ulaya kwa kuifunga Chelsea katika fainali kule Moscow Russia.

Argentina itacheza na Croatia katika mchezo wa kwanza katika michezo miwili ya kirafiki kwa Argentina mchezo utakaopigwa katika dimba la West Ham United ( Upton Park) leo Jumatano kuanzia majira ya Saa 4 na nusu usiku. Ikumbukwe Javier Mascherano na Carlos Tevez walianza kuonekana wakiwa na West Ham hivyo basi itakua muda muafaka kurudi nyumbani.

Siku hiyo Angel Di Maria atakua mwenyeji wa nyota wengine kama Lionel Messi, Sergio Aguero, Cristiano Ronaldo na wengine kibao waliopo kaika vikosi hivyo.

KIKOSI KAMILI CHA ARGENTINA

Makipa:

Sergio Romero (Sampdoria), Wilfredo Caballero (Manchester City), Nahuel Guzman (UANL Tigres)

Mabeki:

Nicolas Otamendi (Valencia), Cristian Ansaldi (Atletico Madrid), Facundo Roncaglia (Genoa), Martin Demichelis, Pablo Zabaleta (both Manchester City), Federico Fazio (Tottenham Hotspur), Federico Fernandez (Swansea City), Ezequiel Garay (Zenit St Petersburg)

Viungo:

 Javier Mascherano (Barcelona), Ever Banega (Sevilla), Roberto Pereyra (Juventus), Lucas Biglia (Lazio), Angel Di Maria (Manchester United), Erik Lamela (Tottenham Hotspur), Javier Pastore (Paris St Germain), Enzo Perez, Nicolas Gaitan (both Benfica)

Washambuliaji:

 Carlos Tevez (Juventus), Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain (Napoli), Sergio Aguero (Manchester City).


++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.