MKUDE SIMBA AONGEZA MIAKA MIWILI KUICHEZEA SIMBA
Kiungo wa Simba ya Dar Es Salaam Jonas Mkude maarufu kama Mkude Simba amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba kufatia mkataba wake wa sasa kuelekea ukingoni.
Jonas Mkude anayeimudu vyema nafasi ya kiungo mkabaji katika timu yake ya Simbana Taifa Stars alikua akinyemelewa pia na Azam FC na Yanga wakitaka kumsajili.
Mbele ya waandishi wa habari Mkude alisaini mkataba huo akiwepo pia Raisi wa klabu hiyo Evans Aveva na Mwenyekiti wa usajili Hans Pope.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments