KUFULIA KUBAYA - KIPA MAARUFU WA ENGLAND DAVID JAMES AANZA KUUZA MALI ZAKE



Aliyekua kipa namba moja wa ENGLAND na klabu kadhaa zinazoshiriki ligi kuu nchini England David James ameanza kuuza baadhi ya vitu vyake zikiwemo jezi alizobadilishana na wachezaji tofauti baada ya ukata mkubwa unaomkabili.


David James ambaye ameichezea England mechi 53 ikiwa ni pamoja na fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini amepiga mnada baadhi ya vitu anavyomiliki vikiwemo gari,mipira,jezi za wachezaji mbali mbali,jezi zake akiwa Porthmouth na timu ya Taifa,vifaa vya mazoezi na vinginevyo.

David James ambaye mwezi May mwaka huu alitangazwa kufirisika anatarajia kupata makusanyo ya mnada huo ambao unamalizika saa 12 jioni leo Jumanne kwa saa za UK sawa na saa 3 Usiku Afrika Mashariki.

Katika vitu vilivyouzwa kwa bei mbaya ilikua ni fulana ya kipa wa Chelsea Petr Cech ambayo kipa huyo wa Chelsea aliivaa katika fainali za kombe la FA mwaka 2010 wakiifunga Portsmouth bao 1-0 ambapo David James alikua kipa wa Pompy siku hiyo. Jezi hiyo ya Petr Cech iliuzwa kwa kiasi cha paundi za Uingereza 3,831 mchana wa leo.

David James ameshauza pia jezi yake aliyovaa wakati wa kombe la dunia akiitumikia England katika kombe la dunia mwaka 2010 dhidi ya Slovenia ambayo iliuzwa paundi 731 baada ya watu kubidi mara 16.

Jezi aliyovaa dhidi ya Ujerumani katika fainali hizo za kombe la dunia  iliuzwa kwa paundi 1,155.

James alianza kufirisika mara baada ya kuachana na mkewe Tanya mwaka 2005 na katika kiwango bora kabisa aliwahi kuzichezea Liverpool,Manchester City na Portsmouth na katika siku za karibuni ameamua kurudi kucheza mpira licha ya kua alishastaafu na sasa ni kocha mchezaji wa timu Kerala Blasters inayoshiriki ligi kuu nchini India.

No comments

Powered by Blogger.