AGUERO KUCHEZA MECHI YA 100 LEO CITY WAKIWAKABILI SOUTHAMPTON
Mkali wa mabao wa mabingwa watetezi wa ligi kuu England Sergio Kun Aguero leo atafikisha mechi yake ya 100 katika Ligi kuu England tangu alipojiunga na mabingwa hao mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid ya Spain.
Aguero anaingia katika historia ya wachezaji waliofunga mabao mengi katika mechi 100 za mwanzo akiwa ameshafunga mabao 64 hivi sasa
Alan Shearer anaongoza orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi katika mechi zao 100 za kwanza katika ligi kuu nchini England alifunga magoli 79 katika mechi 100 akifatiwa na Ruud Van Nistelrooy ambaye alifunga mabao 68 katika mechi 100 na Aguero anakamata nafasi ya 3 akiwa ameshafunga magoli 64
Aguero mwenye miaka 26 tu ameshafunga jumla ya magoli 92 katika mechi 140 katika mashindano yote akiwa na Manchester City.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Huyu Allan shearer alikuwa hatari kwa upachikaji maana ni shider kuhusu wa ligi kuu uingereza yeye anaongoza.
ReplyDeleteAguero kama injury zingemuacha huru nadhani angekuwa na mabao mengi zaid ya haya.
Sure
ReplyDelete