TAIFA STARS VS BENIN LIVE !!!!!
Karibu katika mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Timu ya Taifa ya Benin.
Tutakuletea updates za mechi hii kwa kila kitakachoendelea hapa uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Endelea kua nasi
KIKOSI CHA TAIFA STARS
1. Mwadini Ali
2. Shomari Kapombe
3. Nadir Haroub
4. Erasto Nyoni
5. Aggrey Morris
6. Oscar Joshua
7. Mwinyi Kazimoto
8. Amri Kiemba
9. Haruna Chanongo
10. Mrisho Ngasa
11. Thomas Ulimwengu
AKIBA
Deogratias Munishi
Saidi Moradi
Juma Luizio
Kelvin Yondani
Hamisi Juma
Khamis Mcha
Salum Abubakar
● Mechi itaanza muda si mrefu
■ Mrisho Ngasa anaanzampira hapa ikiwa ni saa 11 na robo
■ Taifa Stars wanapata kona inapigwana Chanongo lakini kichwa cha Canavaro kinaishia mikononi mwa kipa wa Benin
■ Tomas Ulimwengu anakosa bao la wazi hapa kufuatia kazi nzuri ya Mrisho Ngasa aliyekimbia na kupiga krosi
■ Amri Kiemba anajaribu shuti la mbali lakini mpira unapaa juu kidogo ya lango la Benin
■ Dakika ya 8 ya mchezo bado mabao ni bila kwa bila ila Stars wameonekana kuimarika zaidi
■ Taifa Stars imejaza viungo watano katikati huku nyuma kukiwa na mabeki wawili wakati mbele wako Tomas Ulimwengu na Amri Kiemba
■ Dakika ya 15 Benin nao wanaonekana kujiamini
■ ■■■■■■ GOOOOOOOOOOOOOOOOOOLL!!!!!!!!!! ■■■■■■■■■■■■■
■■■■■■■■■■■■■■■■■■■■■■♤♤♤♤♤♤♤■■■■■■■■■■■■■♤♤♤♤
Taifa Stars inapata bao la kwanza Mfungaji ni nahodha Nadir Haroub Canavaro baada ya kuunganisha mpira wa faulo iliyopigwa na Nyoni
■ Goli limefungwa dakika ya 16
■ Mwadin Ali kipa wa Stars anaokoa bao la wazi hapa dakika ya 22 hivi sasa
■ Tomas Ulimwengu anajaribj kupiga shuti nje ya 18 linatoka nje na kuifanya Stars kuwa na madhuti matatu ambayo yametoka nje ya lango
■ Nahodha wa Benin anapata kadi ya njano ni Stephan Sessignon baada ya kutoa maneno makali kwa mwamuzi
■ Tomas Ulimwengu alipiga shuti kali likatolewa na kipa wa Benin ikawa kona ambayo haikuzaa matunda
■ Dakika ya 30 Stars wanapata faulo inapigwa na kubabatiza ukuta wa Benin
■ Benin wanapiga shuti kali langoni mwa Stars lakini linatoka nje ya lango
■ Benin wanapata kona ya kwanza dakika ya 35 ambayo haijazao matunda
naona mabeki wa Stars wameanza kujisahau
■ Dakika ya 38 hivi sasa Kiemba anapiga shuti kali linambabatiza beki wa Benin na kua kona ambayo haikua na madhara
■■■■■■■■■■■ GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOL ■■■■■■■■■■■■■
NI AMRI KIEMBA RAMADHANI ANAIFUNGIA SIMBA BAO LA 2 DAKIKA YA 40 BAADA YA MAKOSA YA BEKI WA BENIN KUMPASIA KIEMBA
STARS 2 - 0 BENIN
MVUA INANYESHA HAPA
■ Dakika ya 45 zimeongezwa dakika 2
■♡♡♡♡♡♡ MPIRA NI MAPUMZIKO TAIFA STARS WANAONGOZA BAO 2-0 ♡♡♡♡♡♡♡
□□□□□□□□□□□□□ DONDOO YA KILICHOTOKEA KIPINDI CHA KWANZA □□□□□□□□□
●● Taifa Stars imepiga mashuti takribani manne katika lango la Benin huku Benin wakipiga shuti moja tu langoni mwa Benin na mashuti yaliyotoka nje pia yalikua hivyo hivyo
●● Taifa Stars imepata kona 3 wakati Benin wamepata kona moja.
●● Taifa Stars imemiliki mpira kwa zaidi ya 53% huku nafasi ya Kiungo ikionekana kuwabana vyema Benin.
■■■■■■■ KIPINDI CHA PILI ■■■■■■■
■■■■■■■ GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOL ■■■■■■■
THOMAS ULIMWENGU ANAANDIKA BAO LA 3 KWA STARS BAADA YA KUUNGANISHA KROSI YA MRISHO NGASA DAKIKA YA 49
■ kadi ya njano kwa Agrey Moris dakika ya 55
■ Anatoka Mrisho Ngasa anaingia Juma Luizio kwa upande wa Taifa Stars dakika ya 58.
■ Sessy anatoka anaingia Ole Fortune kwa upande wa Benin
■ naona mvua imepungua hivi sasa na Watanzania wanashangilia kwa nguvu baada ya Canavaro kuamka alipokua amelala baada ya kugongana na Ulimwengu
■ Salum Abubakar Sure boy anaingia kuchukua nafasi ya Amri Kiemba dakika ya 68 kwa upande wa Taifa Stars
■■ ■■■■■■■ GOOOOOOOOOOOOOOOOL ■■■■■■■■■■
JUMA LUIZIO ANAIFUNGIA STARS BAO LA 4 KUFATIA KAZI NZURI YA THOMAS ULIMWENGU DAKIKA YA 71
■ Benin wanaonekana wamechoka
■ Nadir Haroub Canavaro anatoka hapa nafasi yake inachukuliwa na Said Morad dakika ya 76
■ Said Ndemla anaingia kuchukua nafasi ya Haruna Chanongo upande wa Taifa Stars dakika ya 77
■ Kitambaa cha unahodha kimevaliwa na Erasto Nyoni hivi sasa ikiwa ni dakika ya 84
■ Mpira ni dakika ya 86 hivi sasa Uwanja unaonekana vizuri hapa
■ Taifa Stars wanafanya mabadiliko mengine anatoka Thomas Ulimwengu anaingia Hamis Mcha
■ Zimebaki dakika 2 mpira kumalizika Taifa Stars wanaonekana wamerelax
■ DAKIKA 90 ZIMEMALIZIKA WANAONGEZA DAKIKA 4
■■■■■■■■■♤■■■ GOOOOOOOOOOOOOOOOOL ■■■■■■■
BENIN WANAPATA BAO HAPA KAZI NZURI ILIYOFANYWA NA STEPHAN SESSIGNON INATUMIWA VIZURI NA MSHAMBULIAJI WA BENIN SUANON NA KUANDIKA BAO LA KWANZA
■ Wakati wowote mpira utamalizika hapa mvua inanyesha
■ ♡♡♡♡♡♡♡♡♡♡ MPIRA UMEISHA HAPA UWANJA WA TAIFA DAR TANZANIA INAIBUKA KIDEDEA KWA BAO 4-1 ♡♡♡♡♡♡♡♡♡♡♡
TATHMINI KAMILI YA MCHEZO HUU UTAIPATA MUDA SI MREFU KUPITIA WAPENDA SOKA BLOG
ASANTENI SANA.
No comments