SOUTHAMPTON YAENDELEZA REKODI YA NYINGI NYINGI EPL
..Jana katika ligi kuu england tulishuhudia ushindi wa bao 8-0 walioupata Southampton dhidi ya Sunderland katika dimba la St. Marry's nyumbani kwa Southampton.
Hii si mara ya kwanza pale England kwa timu kufungwa goli 8 au zaidi. Southampton ambao walipoteza wachezaji 6 katika usajili wameanza Ligi wakiwa katika hali nzuri na kushangaza wengine waliodhani watashuka daraja.
Ushindi huo unawaingiza Southampton katika historia ya timu zilizofunga magoli mengi katika mechi moja katika historia ya Ligi kuu England tangu mwaka 1992.
Historia inasema Baadhi ya ushindi mkubwa mwingine ambao umeshawahi kushuhudiwa katika ligi hiyo yani kwa timu moja kufungwa magoli 8 au zaidi ni kama ifuatavyo:-
×××××××××××××××××××××××××××××××××××
- Man United 9-0 Ipswich : May 1995
- Newcastle 8-0 Sheffield Wednesday : Septemba 1999
- Totenham Hotspurs 9-1 Wigan : November 1999
- Chelsea 8-0 Wigan : May 2010
- Chelsea 8-0 Aston Villa :
- Man United 8-2 Arsenal : August 2011
- Southampton 8-0 Sunderland
No comments