SIMBA YACHAPWA 4-2 SAUZI



Simba SC imechapwa bao 4-2 na timu ya Chuo kikuu cha Wits katika mwendelezo wa mechi za kujiandaa na pambano dhidi ya watani wao wa Jadi Yanga Jumamosi hii, pambano litakalopigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.

Ilikua ni nafasi nyingine kwa Simba kumtumia kipa wake namba 3 Peter Manyika ambaye ni mtoto wa Kipa wa zamani wa Yanga Peter Manyika na hii ni kutokana na Makipa Ivo Mapunda na Hussein Shariff kuwa majeruhi.



Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Starock Park jijini Johannesburg Afrika Kusini magoli ya Simba yalifungwa na Ramadhani Singano (Messi) aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Uhuru Suleiman huku goli lingine  likifungwa na mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka JKT Ruvu Elias Maguri.

Kikosi cha Simba leo kilikua hivi:-

Peter Manyika,
Willam Lucian, Mohamed Hussein,Abdul Aziz, Joseph Owino,Pierre Kwizera,Twaha Ibrahim,Abdallah Sesseme,Elias Maguri,Shaban Kisiga na Uhuru Selemani.

Walioingia kutokea benchi ni :-
Ramadhani Singano 'Messi'
Amis Tambwe
Ibrahim Ajibu

Wakati Huo Huo Timu ya Yanga Imeingia kambini katika Hotel ya Landmark iliyoko Kunduchi jijini Dar es salaam kujiandaa na pambano hilo ambalo huvuta hisia za mashabiki wa Soka Nchini.

... Edo Daniel Chibo

No comments

Powered by Blogger.