HABARI 8 KALI ZA SOKA LEO JUMATATU
NYUMBANI
1. Shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF limemfungia wakili Damas Ndumbaro kwa miaka 7 kutojihusisha na Soka ndani na nje ya nchi kufuatia hatua ya uchochezi kuhusu swala la klabu za Ligi kuu kuchangia 5% ya Maendeleo ya soka la vijana.
2. Klabu Ya Simba ya Jijini Dar es Salaam leo imepokea kichapo cha bao 4-2 toka kwa timu ya Wits University katika kambi yake huko nchini Afrika Kusini.
Magoli ya Simba yalifungwa na Ramadhan Singano na Elias Maguli.
3. Klabu Ya Yanga imeanza kambi yake ya mazoezi kujiandaa na pambano dhidi ya Simba kwa kuweka kambi kando ya jiji la Dar Es Salaam katika hoteli ya Landmark Kunduchi.
4. Jamhuri Kiwelu 'Julio' na kikosi chake cha Mwadui FC wameshawasili mjini Moshi tayari kwaajili ya pambano lao la ligi Daraja la Kwanza Tanzania bara dhidi ya Pannone FC ya Moshi.
ULAYA
5. Taarifa njema kwa mashabiki wa Arsenal kwani mshambuliaji Theo Walcot amerudi katika mazoezi ya timu yake hiyo baada ya kukaa nje ya uwanja Tangu mwezi wa kwanza alipoumia goti katika mchezo dhidi ya Totenham Hotspurs
6. Goli pekee la Wayne Rooney liliipa ushindi mwembamba England katika mechi dhidi ya Estonia ugenini na kuwafanya vijana hao wa Roy Hudgson kuongoza kundi E wakiwa na pointi 9 baada ya michezo miatatu.
6. Majeruhi yaliyokua yakivizungua Vilabu vingi vya Soka barani Ulaya yanaanza kupata ahuweni kwa wachezaji hao kurudi mchezoni na mmoja wao ni Kiungo wa Borussia Dortnund Ilkay Gundogan baada ya kukaa nje ya dimba muda mrefu anarudi uwanjani sasa na pengine kocha Jurgen Klopp atampanga katika mchezo dhidi ya FC Kolon
7. Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amefunguka na kuomba msamha kwa kitendo cha kumsukuma kocha Jose Morinho katika mchezo Wa Ligi Kuu Nchini England ambapo Arsenal walikubali kichapo cha bao 2-0 toka kwa Chelsea.
8. Beki wa AS Roma Doglas Maicon ameongeza mkata wa mwaka mmoja wa kuichezea klabu hiyo yenye maskani yake katika jiji la Roma nchini Italia.
... Kwa leo tuishie hapa tukutane tena kesho
Nawatakia usiku Mwema
Imeandaliwa na Edo Daniel Chibo
.......Usisahau ku like ukurasa wetu Facebook (Wapenda Soka- kandanda)
No comments