SIMBA NA YANGA ZASHINDA MECHI ZAO ZA KIRAFIKI LEO



Watani wa jadi katika soka la Bongo Simba na Yanga leo walishinda bao 1-0 katika mechi zao za kirafiki.
Simba ikiwa Mjini Iringa iliivurumisha Lipuli ya huko ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza Tanzania Bara kwa bao 1-0  katika pambano lililofanyika katika dimba la Samora mjini Iringa.Goli la Simba likifungwa na Elias Maguli.




Simba wameweka kambi Iringa kujiandaa na mchezo wao wa Jumamosi hii dhidi ya Mtibwa Sugar mjini Morogoro na hii ni baada ya kutoka sare na Prisons katika pambano lililopigwa Jumamosi iliyopita katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Kwa upande wao Yanga waliifunga timu ya Ambassador ya mjini Kahama bao 1-0 goli pekee la mchezo huo likifungwa na Said Bahanuz.
Yanga wameweka kambi ya muda mfupi katika mji wa Kahama ikijiandaa na pambano la Jumamosi dhidi ya Kagera Sugar.

Yanga itaingia katika mchezo wa Jumamosi ikiwa inafurahia udhindi wa bao 3-0 walioupata Jumamosi dhidi ya Stand United katika uwanja wa Kambarage.

××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××

No comments

Powered by Blogger.