NAZIDIWA NA WACHEZAJI WATANO TU DUNIANI ~ EDEN HAZARD
Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard anaamini kuwa yeye ni bora duniani kwasasa na anazidiwa na wachezaji watano tu ambao ni Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, Lionel Messi wa Barcelona, Zlatan Ibrahimovic wa PSG, Frank Ribbery na Arjen Roben wa Bayern Munich.
Hazard aliyekua mchezaji bora wa mechi baina ya timu yake na Arsenal anasema kazi iliyoko mbele yake ni kuisaidia Chelsea kushinda makombe na yeye kufikia level za hao wanaompita. Hazard anaamini hao ni wachezaji pekee ambao wanaweza kubadilisha hali ya mchezo muda wowote wawapo uwanjani.
Chelsea inaongoza katika msimamo wa ligi kuu nchini England ikiwa imeshajikusanyia pointi 19 baada ya kucheza michezo 7 ikishinda 6 na kutoka sare 1 huku ikiwa imefunga magoli 14 mpaka sasa.
Chelsea ndiyo klabu pekee ambayo haijafungwa mchezo wowote katika ligi na mpaka sasa inashiriki mashindano yote ikiwemo ligi ya mabingwa Ulaya, Ligi kuu England na kombe la ligi nchini England (Capital One)
Unadhani ni kweli Hakuna mchezaji mkali anayemzidi Hazard hivi sasa katika kusakata kabumbu ukiacha hao aliowataja?
×××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××
ADM7 anamzidi pia
ReplyDelete