HIVI NDIVYO MAMA YAKE ADIN DZEKO ALIVYOMWOKOA MWANAE NA KIFO

Edin Dzeko.

Mkali wa mabao Raia wa Bosnia Hezgovina , mwenye miaka 28 anayekipiga katika klabu ya Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi kuu England (EPL).
Ni kati ya wachezaji wachache wanaojua lugha nyingi kwani Dzeko anaongea vizuri lugha ya Kibosnia, Kiczech, Kijerumani na Kiingereza.

Historia ya mchezaji huyu katika soka imetawaliwa na mambo mengi ya kusikitisha kwani Amecheza sana mpira wa mtaani kama walivyo wachezaji wengi ila bahati mbaya kwake amekulia kwenye nchi iliyopigana vita ya wenyewe kwa wenyewe
enzi hizo ikiitwa Yugoslavia.
Sarajevo ndo mji aliokulia, mji uliokumbwa na machafuko ya kisiasa kwa mda mrefu kupelekea watu wengi kupoteza  maisha yao.

Mama yake, Belma anasema Edin alikua mtundu sana, alikua akimkataza kwenda kucheza mpira viwanjani, kwa sababu mabomu yalikua yanapigwa hasa sehemu za halaiki. Lakini Edin alikua akipenya kwenye fensi, akisubiriwa na wenzake, na wanaenda viwanjani kusakata soka ambalo leo limemfanya awe milionea.



Siku moja, mama yake Edin, alimfungia mwanae huyo, ndani, akampa chakula na kumuwashia televisheni. Edin alilaani na kulia sana akisema mechi hiyo ilikua ni muhimu asingeweza kukosa. Hata chakula alizira kula siku hiyo kumuonyesha mama yake kama alikwazika.

Ni maamuzi ambayo kwa namna moja au nyingine yameitengeneza "career" ya Edin na kumweka hai mpaka leo.
Hiyo ndiyo siku ambayo ilihifadhi mambo mengi tunayoyaona hivi sasa kwa Edin Dzeko kwani ni siku ambayo kiwanja alichozoea kucheza Edin na wenzake, kilipigwa mabomu ya angani, na watoto wote waliokua uwanjani hapo wakifurahia soka  walifariki baada ya kupigwa na mabomu hayo. Na moja kati ya waliokufa  alikua ni binamu yake Edin Dzeko aliyejulikana kwa jina la Alexanda Dzeko.
Dzeko wa nne toka kushoto  waliochuchumaa

Baada ya tukio hilo Mama yake alimpeleka kanisani, na wakasali sana, akiamini Mungu ana mipango  na mwanae.
 Baadae alipata bahati ya kwenda kusoma nje ya nchi na hapo ndipo alipotokea.

Leo hii  Edin Dzeko ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha kifahari cha Manchester City kikosi ambacho amekiongoza kushinda makombe mawili ya Ligi kuu nchini England, ameshinda pia Kombe la ligi (Capital One), kombe la FA mara moja na Ngao ya jamii mara moja
Amewahi pia  kutwaa ubingwa wa Ujerumani na club ya Wolfsburg msimu wa 2008/2009. Yeye akitwaa kiatu cha mfungaji bora, akifunga magoli 30.

HUYU NDO EDIN DZEKO


{ Fankinho WS}

No comments

Powered by Blogger.