WACHEZAJI YANGA NA AZAM WATAWALA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA



KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij ameteua wachezaji 26 kwa ajili mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kocha Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), safu ya ulinzi itaendelea kutegemea mabeki wa Yanga SC kwa mujibu wa kikosi alichoteua ambacho kitaingia kambini Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es salaam

Wachezaji walioitwa ni :-




MAKIPA

 Deogratias Munishi (Yanga),
 Aishi Manula (Azam),
 Mwadini Ali (Azam).

MABEKI

 Said Moradi (Azam),
 Shomari Kapombe (Azam),
Oscar Joshua (Yanga),
Nadir Haroub (Yanga),
Kelvin Yondani (Yanga),
Aggrey Morris (Azam),
Miraji Adam (Simba),
Charles Edward (Yanga)
 Emmanuel Simwanda (African Lyon).

VIUNGO

Erasto Nyoni (Azam),
Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar),
 Amri Kiemba (Simba),
Himid Mao (Azam),
 Salum Abubakar (Azam),
Said Ndemla (Simba)
 Haruna Chanongo (Simba).

Washambuliaji

Khamis Mcha (Azam),
Simon Msuva (Yanga),
 Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo),
Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo),
 Mrisho Ngasa (Yanga),
Mwegane Yeya (Mbeya City),
 Juma Liuzio (Zesco, Zambia).

Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.