TATHIMINI YA MECHI: MAN UNITED VS QPR



Hali imeanza kutulia katika kikosi cha Manchester United  baada ya kupata ushindi wa bao 4-0 ukiwa ni ushindi wa kwanza kwa kocha mpya Luis Van Gaal katika ligi kuu England.
 Luis Van Gaal akitumia wachezaji wake wote aliowanunua kipindi hiki walionekana kuendana na mfumo wa sasa wa Man United.
Baada ya kusumbuka na mfumo wa 3-5-2 kocha wa Man United aliamua kubadilika na kucheza mfumo wa Diamond lengo likiwa ni kuwatumia wachezaji wake wote hapo Di Maria,Mata,Rooney,Falcao na Van Perse



Ikambidi kutumia mfumo wa 4-1-2-1-2 wakianza nyuma Rafael na Rojo beki za Pembeni huku Blacket na Evans wakisimama beki za kati.
Daley Blind alikua na kazi moja tu ya kutibua mipango ya QPR wakati Ander Herrera,Di Maria na Mata walikua wakipenyeza mashambulizi kupitia kila njia pembeni hasa hasa kwa Di Maria.
Mbele walisimama Rooney na Van Perse.

Pengine wengi watasema QPR si timu ya kujisifia lakini LVG anatambua hizi ndo mechi za kujaribu mfumo.
Kitu ambacho niliona amejihatarisha ni kuwachezesha Falcao,Rooney na Van Perse pamoja dakika za mwisho kwani mashambulizi yalipungua tofauti na alipokuwepo Mata.

Tathmini ya kilichotokea katika mchezo huo ilikua kama ifuatavyo:-

■ MAN UNITED 4-0 QPR

■ WAFUNGAJI
Angel Di Maria 24'
Ander Herrera 36'
Wayne Rooney 44'
Juan Mata 58'

■ TAKWIMU MUHIMU:
>  ● Mashuti yaliyolenga goli
    : Man United 10-2 QPR
> ● Mashuti yaliyotoka nje ya goli
     : Man United 6-3 QPR
> ● Kona
    : Man United 3-1 QPR
> ● Faulo
    : Man United 11-8  QPR
> ● Kadi za Njano
    : Man United 1-0 QPR
 >  ● Umiliki wa Mpira
     : Man United 69%-31% QPR

MAN OF THE MATCH - ANGEL DI MARIA
Huyu jamaa kaonyesha kwanini Madrid walikosea kumruhusu aondoke. Pasi zake na jinsi alivyokua akiisumbua ngome ya QPR na alihusika katika kila goli walilofunga United
×××××××××××××××××××××××××××××××××××××××

{ Edo DC }

No comments

Powered by Blogger.