TAMBWE ATISHIA KUONDOKA SIMBA



STRAIKA mahiri wa Simba,Amissi Tambwe, amesema alisikitishwa na taarifa za yeye kutaka kuondolewa kikosini ili kumpisha Emmanuel Okwi raia wa Uganda katika kikosi cha Simba na kuongeza kuwa anasubiri usajili wa dirisha dogo ili afanye uamuzi mgumu.

Uongozi wa klabu ya Simba ulikuwa unafikiria kumchomoa kikosini hapo baada ya kutakiwa kupunguza mchezaji mmoja wa kigeni kumpisha Okwi ili kukidhi idadi ya wachezaji watano wa kigeni wanaoruhusiwa kucheza katika klabu moja.



Simba tayari ilikuwa na Joseph Owino raia wa Uganda, Donald Mosoti na Raphael Kiongera raia wa Kenya pamoja na Warundi Pierre Kwizera na Tambwe hivyo kutakiwa kumpunguza mmoja. Mosoti ndiye aliyekuja kuondolewa baadaye baada ya hoja ya Tambwe kupata upinzani mzito.

“Siwezi kuweka wazi klabu nilizotaka kwenda lakini nilikuwa na mipango mingi, kwa sasa nasubiri dirisha dogo ili niweze kukamilisha mipango yangu, mimi naifahamu kazi yangu na huwa sichezi kwa kubahatisha,” alisema Tambwe.

Hata hivyo straika huyo alizungumzia swala la Musoti kuondoka Simba na mabeki waliopo hivi sasa na kusema “Mosoti tayari ameshaondoka, hakuna ujanja hao vijana wanatakiwa wajitahidi kucheza kwa kuelewana na kuisaidia timu, hapo tutasogea lakini ukweli ni kwamba kuna vitu vya Mosoti ambavyo tutavikosa.

#Chardboy

××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××

No comments

Powered by Blogger.