TAIFA STARS YAPAA LEO KWENDA BURUNDI KWA PAMBANO LA KIRAFIKI


Wachezaji 20 wa timu ya taifa (Taifa Stars) wameondoka nchini leo alfajiri kwenda Bujumbura, Burundi kwa ajili ya mechi ya kimataifa ya kirafiki itakayopigwa siku ya Jumapili dhidi ya kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi Maarufu kama 'Etamba Murugamba'

Kikosi cha Stars kikiwa chini ya kocha Mholanzi Mart Nooij na msaidizi wake Salum Mayanga kinaondoka kikiwa na matumaini ya kulipiza kisasi cha kufungwa 3-0 siku ya sherehe za Muungano katika uwanja wa Taifa April 26 Mwaka huu.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuagwa kwa Taifa Stars, Nooij alisema amekiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha kinaibuka na ushindi ili kulipa kisasi cha kufungwa nyumbani na pia kujihakikishia kupanda katika viwango vya soka vya kimataifa vinavyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
"Ninatambua Burundi ina wachezaji wazuri na wa kimataifa kina (Amisi) Tambwe (Pierre) Kwizera na (Didier) Kavumbagu lakini kwa kikosi tunachokwenda nacho, tuna uhakika wa kushinda ugenini na kulipa kisasi maana walitufunga kwetu," alisema Nooij.

List ya wachezaji 20 walioondoka leo alfajiri ni pamoja na:-

MAKIPA
Mwadin Ally (Azam FC)
Deogratias Munishi 'Dida' (Yanga).

MABEKI
Shomari Kapombe (Azam FC),
Oscar Joshua (Yanga),
Said Morad (Azam FC),
Nadir Haroub 'Canavaro' (Yanga) ,
Kelvin Yondani (Yanga),
Joram Mgeveke (aliyesajiliwa Simba kutoka kikosi cha Maboresho ya Taifa Stars),

VIUNGO
Simon Msuva (Yanga)
Erasto Nyoni (Azam FC),
Himid Mao (Azam FC),
 Amri Kiemba (Simba),
Haruna Chanongo (Simba),
 Salum Abubakary 'Sure Boy' (Azam FC),
Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya ya Qatar),

WASHAMBULIAJI
Hamis Mcha (Azam FC),
Juma Luizio (Zesco FC, Zambia),
Mrisho Ngasa (Yanga),
Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC)
Thomas  Ulimwengu ( TP Mazembe, DRC).

Kwa upande mwingine Mshambuliaji na nahodha wa Azam FC, John Bocco 'Adebayor', beki Agrrey Morris na kipa Aishi Manula wameachwa katika msafara wa Burundi kwa sababu mbalimbali zikiwamo majeraha na kutokuwa na uhakika wa kucheza Jumapili.

~ Edo Daniel Chibo
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.