MAGOLI 14 YA PENATI YAIVUSHA LIVERPOOL CAPITAL ONE



Iliwabidi Liverpool kupiga penati 14 mpaka kuwang'oa Middlesbrough katika Kombe la Ligi nchini England maarufu kama Capital One raundi ya 3.

Mchezo huo ulipigwa katika dimba la Anfield nyumbani kwa Liverpool ulikua mgumu kwa Liverpool licha ya kutangulia kufunga bao dakika ya 10 tu ya mchezo likifungwa na Jordan Rossiter kabla ya Middlebrough hawajasawazisha dakika 63 kupitia kwa Adam Reach.

Mpaka mchezo unaisha Liverpool 1-1 Middlebrough,Matokeo ambayo yakaipeleka mechi hiyo kuongezwa muda mpaka dakika 120 ambapo Liverpool kupitia kwa mchezaji wake Suso walifunga bao la 2 dakika ya 109. Wakati wengi wakiamini Liverpool atashinda Middlesbrough walipata bao dakika ya mwisho kwa njia ya penati likifungwa kwa njia ya penati na Patrick Bamford hivyo kuamriwa kupigwa mikwaju ya penati baada ya matokeo ya mwisho kuwa 2-2.

Kwa hali isiyotegemewa Timu zote zilipata penati zao 5 za mwanzo hivyo ikabidi ziongezwe moja moja  mpaka zilipofikia 14 ndipo kikosi cha Kocha Brendan Rodgers wakahesabu ushindi kwani wakapata penalt yao ya 14 wakati Middlesbrough wakakosa. Hivyo Liverpool wamevuka hatua hii ambapo sasa watapangiwa timu ya kukutana nayo katika raundi inayofata.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++×++++++++++

No comments

Powered by Blogger.