ALICHOSEMA OKWI KUHUSU MSHABIKI WA YANGA
Na Allen Kaijage
Mahojiano na Rama Salim
Baada ya mechi ya Simba na Coastal Union nilifanikiwa kuongea na Okwi
kwa upande wa Simba na Rama Salim kwa upande wa Coastal. Emmanuel Okwi alihusika kwenye magoli yote
ya Simba, kama ilivyo kwa Rama Salim naye alihusika kwenye magoli yote ya
Coastal union kwa kupika goli moja na kufunga lingine.
Mahojiano na Rama Salim
Nilianza mahojiano yangu na Rama Salim mchezaji wa zamani wa
Gor mahia ya Kenya ambaye mwaka 2011 alikua mchezaji bora chipukizi wa ligi kuu
ya Kenya almaarufu KPL.
Mwandishi: Rama hongera kwa kazi nzuri uliyoifanya leo.
RAMA: Ahsante sana.
Mwandishi Kaijage akiwa na Rama Salim |
Mwandishi: Rama kipindi cha kwanza hamkucheza vyema, unadhani ni kwanini?
RAMA: Ujue Simba ni timu kubwa, kipindi cha kwanza tulikua
na ‘Tension’ ila kadiri mchezo ulivyokua unaendelea na ujasiri ulikua unaongezeka.
Mwandishi: Nini kiliwafanya mbadilike kipindi cha pili?
RAMA: Maneno ya kocha baada ya kipindi cha kwanza
kumalizika.
Mwandishi: Umejipangaje kwenye mechi zijazo?
RAMA: Nitajitahidi kufanya vizuri zaidi.
Mwandishi: Ahsante na kazi njema
RAMA: Kazi njema na wewe.
Mahojiano na Emmanuel Okwi
Baada ya mahojiano na Rama nilikaa dakika kadhaa kumsubiri
Okwi aliyekuwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Emmanuel Okwi akatoka huku akiwa anaonekana
mwenye haraka, Ilibidi na mimi niongeze kasi ili nipate mawili matatu kutoka
kwake.
Mwandishi: Habari ndugu Okwi?
Okwi: salama kaka.
Mwandishi: Okwi unazungumziaje kiwango chako na cha timu kwa ujumla.
Okwi: Mara nyingi sipendi kuzungumzia kiwango changu binafsi
kuliko cha timu. Tulicheza vizuri kipindi cha kwanza na Coastal walicheza
vizuri kipindi cha pili.
Mwandishi: Kama mchezaji utafanya nini ili mechi ijayo timu
yako ipate Ushindi
Okwi :Ujue sijafurahia sana kiwango nilichoonesha leo, nitajitahidi
kuongeza mazoezi ili mechi ijayo niisaidie timu yangu kupata ushindi.
Mwandishi: Unajisikiaje kwa kitendo cha mashabiki wa Yanga
kukuzomea kila unapogusa mpira?
Okwi: Sina muda nao, mimi sasa ni mchezaji wa simba, mambo
yote kuhusiana na yanga hayanihusu.
No comments