KAIJAGE NA SUSO KATIKA UTABIRI WA LIGI KUU ENGLAND



Tottenham vs Liverpool : 15:30

Mauricio Pochetino vs Brendan Rodgers

Uzuri wa kwanza wa hii mechi ni falsafa za hawa makocha wawili hawana tofauti sana, wote wanataka timu icheze mpira mzuri na ifunge. Pengine Liverpool ndio itakaribisha dimbani nyota wake wote iliowasajili msimu huu. Ingawa jicho na sikio la mpenzi yoyote wa Liverpool likiwa kwa atakachofanya Mario Balloteli maana huyu ndie atakaeweka matumaini ya mashabiki hai au kuyazorotesha lakini bado nadhani silaha Yao itategemeana kuelewana kwao  na ninaona Markovic akiwa na siku nzuri kama akicheza. Totenham wameanza msimu vyema sana na Mauricio inaonakena anakipatia kikosi kuanzia namna ya uchezaji mpaka matumizi ya wachezaji wenyewe sidhani kama itakuwa mechi rahisi hasa kwa Liverpool.
Utabiri:



Suso Tot 1 Liverpool 1
kaijage Tot 1 Liverpool 2


Leicester Vs Arsenal : 18:00

Bado itaendelea kuwa ratiba ngumu sana kwa hii timu iliyopanda daraja, ni ratiba itakayokuwa ya kuwachosha kwa kipindi hiki. Arsenal wanatoka kupata ushindi katika mchuzo wa ligi ya mabingwa, Aaron Ramsey ambaye kwangu namuona kama Lampard mpya katika kufunga anarejea, hii itakuwa mechi nzuri sana ukizingatia aina ya uchezaji ya Leicester wakiwa nyumbani. Alexis Sanchez, amekuwa kimya kiasi lakini ndio wakati wake wa kuonyesha thamani yake huku Mesut Ozil akitakiwa kurejesha makali yake. Vinginevyo Arsenal inabidi washindane na kasi ya Leicester wakiwa na mpira na presha ya ule uwanja, nawaona wakiruhusu goli.
Utabiri:

Suso: Leicester 1 Arsenal 2
kaijage Leicester 0 Arsenal 2

Aston Villa vs Hull City : 15:30
Kwa upande wa Aston Villa nadhani kurejea kwa goli kipa wao Brad Guzan katika milingoti na beki Vlaar kutawapa khali ya kujiamini zaidi na kucheza vyema zaidi. Wakiwa nyumbani nadhani mechi ambayo Fabian Delph inabidi aitendee haki thamani ya kuitwa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza. Naamini huyu Ndo mwenye matokeo kwa kiasi Fulani ya Asto Villa. Hull city watawategemea watu wao walewale na kurejesha kikosini akina Huddlestone na Ince. Itakuwa ni mecho ngumu yenye kuhitaji matokeo.
Suso: Astonvilla 1 Hull city 0

Kaijage Astonvilla 2 Hull city 1


~ Imetayarishwa na Allen Kaijage na Nicasius Coutinho Suso toka Wapenda Soka group fb...

No comments

Powered by Blogger.