ARSENAL NA NAPOLI ZABANWA LIGI YA MABINGWA ULAYA
Hatua ya kwanza ya mchujo ya kuwania nafasi ya kuingia katika makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya imezishuhudia Arsenal na Napoli zikitoka sare na kusubiri mechi za marudiano kuamua kama zitavuka hatua hii.
![]() |
Wilshere akipambana na Koybas |
Wakiwa Ugenini Arsenal waliweza kuwabana vilivyo Besiktas na kupata sare hiyo licha ya Aaron Ramsey kupewa kadi ya nyekundu baada ya kupata kadi mbili za njano. Besiktas ambao walikua wakiongozwa na Demba Ba walifanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Arsenal huku wakionekana wametulia vilivyo.
Arsenal sasa Itasubiri mechi ya wiki ijayo Jijini London kuangalia kama watavuka hatua hii ambayo miaka yote wamekua wakivuka na kuingia hatua ya makundi.
![]() |
Higuain akifurahia baada ya kuisawazishia timu yake |
Napoli wao wakiwa Nyumbani walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Athletic Bilbao ya Spain huku Bilbao wakitangulia kufunga goli dakika ya Iker Munian kabla ya Gonzalo Higuain hajasawazisha dakika ya 68.
MATOKEO KAMILI YA MECHI ZOTE ZA JANA
- Besiktas 0-0 Arsenal
- FC Koebenhavn 2-3 Bayer Leverkusen
- SSC Napoli 1-1 Athletic Bilbao
- Salzburg 2-1 Malmo FF
- Steau 1-0 PFC Ludogorets
- Aalborg vs Apoel Nico
- Bratislava vs BATE
- Lille vs Porto
- Maribor vs Celtic
- St. Liege vs Zenit
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments