LIGI KUU TANZANIA BARA HATUA YA LALA SALAMA ~ TIMU GANI ITACHEKA?
Hatua ya lala salama ya Ligi kuu Tanzania Bara inataraji kuanza leo na kesho ambapo timu zote 14 zitakua zikitafuta pointi 3 muhimu ili kujiimarisha.
Mabingwa Watetezi Yanga "Wazee wa Uturuki" watakua Uwanja wa taifa Dar Es Salaam kuikaribisha Ashanti ya Ilala ambayo inanolewa nanAbdallah Kibaden aliyekua kocha wa Simba wakati ligi ikianza mzunguko wa kwanza.
Azam itaikaribisha Mtibwa Sugar katika pambano linaolotarajiwa kuwa la upinzani mkali katika uwanja wa Azam Complex pale Chamazi.
Mechi zingine itashuhudiwa Coastal Union wataialika JKT Oljoro katika uwanja wa Mkwakwani. Mbeya City wanaokamata nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi wamesafiri kuivaa Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba.
Simba wao wataialika Rhino ya Tabora hapo kesho katika uwanja wa Taifa wakati Jkt ruvu wataikaribisha Mgambo katika uwanja wa Chamazi siku ya kesho.
Yanga wanaongoza Ligi hiyo wakiwa na pointi 28 ikifatiwa na Azam Yenye point 27 sawa na Mbeya City. Simba iko nafasi ya 4 ikiwa na point 24 huku Mgambo wakikamata mkia wakiwa na point 6.
Kila timu imejiandaa vyema kufanya vizuri mzunguko huu swali ni Je timu ipi itaibuka Kidedea?
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

usiulize embe Kibada hapo bingwa ni YANGA...
ReplyDeletehehehehehehehe
ReplyDelete