LIGI KUU ENGLAND ~ SHUJAA OLE KUKARIBISHWA "WAKATI" MBAYA. LIVERPOOL NA EVERTON HAPATOSHI

Ligi kuu ya England inaendelea Usiku huu kwa viwanja sita kuwa katika wakati mgumu.
Hebu tuangalie kwa kifupi mechi hizo ambazo zitapigwa leo
  • 22:45 MAN UNITED vs CARDIFF CITY
Mashabiki wa Man United Duniani wanasubiri kumwona Shujaa Ole Gunnar Solskjaer akirejea Old Trafford akiwa kama Kocha wa Cardiff City timu iliyo katika nafasi ya mwisho katika ligi.

Pengine huu si wakati muafaka sana kwa Ole kucheza katika uwanja uliompa mafanikio mengi likiwemo goli la dakika ya mwisho lililowapa ushindi United dhidi ya Bayern Munich katika kombe la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kocha Sir Alex Ferguson, kwani United leo wanahitaji ushindi zaidi kuliko heshima kwa Ole.

Ole ni mchezaji aliyependwa na mashabiki na kuipa mafanikio timu hiyo ambayo ni mabingwa Watetezi wa ligi hiyo kwani akiwa Old trafford aliweza kufunga magoli 126 katika michezo 366.

Pia mashabiki watasubiri kumwona Juan Mata mchezaji aliyevunja Rekodi ya Usajili ya klabu hiyo akitokea Chelsea akicheza kwa mara ya kwanza akiwa katika jezi nyekundu. 
Robin van Perse, Wayne Rooney na Maroane Fellain wanataraji kurudi katika mechi hii baada ya kufanya mazoezi na timu tangu jana.

Ushindi kwa Man United  leo utaifanya klabu hiyo kuwa klabu ya kwanza katika historia ya Ligi kuu England kufikisha point 1,000 katika michezo yake ya Ligi.
Mechi ya mwisho baina ya timu hizo iliisha kwa sare ya bao 3-3 katika uwanja wa Cardiff City.

  • 23:00  LIVERPOOL v EVERTON
Hii ni dabi ya jiji la liverpool kati ya mahasimu wa jadi wa jiji hilo Liverpool inayokamata nafasi ya 4 ikiikaribisha Everton iliyo katika nafasi ya 6.
Hii mechi imekuja wakati mbaya kwa timu zote baada ya kutawaliwa na majeruhi wengi.
Joe Allen na Mamadou Sakho wako katika hatihati kuacheza mpambano wa leo baada ya kusumbuliwa na misuli ya paja. Wachezaji wengine wa Liverpool walio katika majeruhi na wataikosa mechi hii ni pamoja na Jose Enrique, Daniel Agger, Lucas Leiva na Glen Johnson.

Everton wenyewe wako katika hatihati ya kuwatumia baadhi ya wachezaji ambao wamekua majeruhi na mpaka sasa kuna uwezekano mkubwa ikawakosa Phil Jagielka, Sylvain Distin, Antolin Alcaraz, Seamus Coleman, Ross Barkley na Steven Pienaar huku Byan Oviedo pengine hatocheza tena mpaka msimu ujao.

 Timu zote hizi ziko kati ya timu zenye nafasi ya kuchukua ubingwa kwa tofauti ya pointi walizonazo pamoja na Arsenal wanaoongoza ligi.

Liverpool Haijawahi kufungwa katika mechi 13baina ya timu hizo katika ligi wakishinda mechi 6 na kutoa sare mara 7 na mara ya mwisho Everton kushinda ilikua mwaka 1999.
Mechi kati ya miamba hiyo ya Jiji la Liverpool imezalisha kadi nyekundu 20 katika michezo ya Ligi kuu.

Steven Gerard ndiyo mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi kati ya timu hizo akifunga magoli 7 mpaka sasa katika ligi.
Kocha wa Everton Roberto Martinez kama atashinda leo atafikisha ushindi wake wa 100 katika Ligi kuu huku Nahodha Phil Jagielka akicheza mechi yake ya 200 leo kama atapangwa.

  •  22:45 SOUTHAMPTON v ARSENAL
Hii ni mechi nyingine tamu kuiangalia leo Arsenal wanaoongoza ligi watasafiri kuikabili Southampton huku Ushindi pekee ukihitajika ili kuongeza wigo wa pointi katika uongozi wa Ligi.

Arsenal wanataraji kuwakaribisha kikosini Aaron Ramsey , Mikel Arteta na nahodha Thomas Vermaelen huku Jack Wilshere akikosekana kutokana na maumivu ya Enka.
Southampton wao wanataraji kuwakaribisha kikosini tena Rickie Lambert na kipa Artur Boruc waliokua wagonjwa wakati Victor Wanyama aliyekua nje kwa matatizo ya Enka anaweza kurudi lakini  Dejan Lovren na Gaston Ramirez wataikosa mechi hii wakiwa majeruhi.

Katika mechi 9 zilizopita baina ya timu hizo Arsenal imeibuka kidedea mechi zote ikipoteza mara ya mwisho mwaka 2002 katika ligi na mechi ya mwisho katika uwanja wa St.Mary's timu hizo ziliisha kwa sare ya 1-1.

Southampton wana pointi 31 katika mechi 22 walizocheza msimu huu haya yakiwa mafanikio kwa timu hiyo tangu msimu wa 2002-2003 ambapo walikua na point 35 na kumaliza msimu katika nafasi ya 8.
  
 
Kwa upande wao Arsenal wana pointi 51 mpaka sasa baada ya mechi 22 mara ya mwisho kufikia mafanikio kama haya baada ya mechi 22 katika ligi ilikua msimu wa 2003-04 walipomaliza msimu mzima bila kufungwa.

MECHI ZINGINE USIKU HUU NI PAMOJA NA
  •  SWANSEA v FULHAM   22:45
  • CRYSTAL PALACE v HULL CITY 23:00
  • NORWICH v NEWCASTLE 22:45
Imetayarishwa na Edo Daniel Chibo
+++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.