FA CUP ~ NI VITA YA MORINHO NA PELLEGRIN WAKATI ARSENAL WAKO NA LIVERPOOL

Raundi ya 5 ya Kombe la chama cha soka nchini England maarufu kama Kombe la FA imepangwa na huku ikishuhudiwa vigogo vya soka la England vikipangwa kucheza pamoja.

Kinara wa ligi hiyo Arsenal wataWataikaribisha Liverpool huku Chelsea wakisafiri mpaka Jiji la Manchester Kuikabili timu inayoogopwa hivi sasa hasa ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani Manchester City.
Baada ya droo hiyo kocha wa Chelsea alinukuliwa akisema "Ili uwe bora lazima uzifunge timu bora,Hivyo ni vizuri kwetu nategemea itakua mechi nzuri"

Kwa ratiba ilivyo Arsenal watasafiri kucheza na Liverpool katika Ligi kabla ya Kurudi nyumbani kuikaribisha Man United halafu watasafiri tena kuikabili Liverpool katika kombe la FA.

Ratiba kamili ya Kombe la FA imepangwa kama ifuatavyo:-
  • Man City v Chelsea
  • Liverpool v Arsenal
  • Brighton v Hull City
  • Cardiff City v Wigan
  • Sheffield Wednesday v Charlton Athletic
  • Sunderland v Southampton
  • Everton v Swansea City
  • Sheffield United or Fulham v Nottingham Forest or Preston North End
...... Mechi hizo zitapigwa wikiendi ya Tarehe 15 na 16 Februari mwaka huu.

+++++++++++++++++++++++++++++++++

1 comment:

  1. Acha umbulula basi? Habari si ya kwako umekopi na kupaste then unajifanya ni ya kwako sio? Poor thnking capacity shenzi ww

    ReplyDelete

Powered by Blogger.