THE GUNNING MACHINE YA MWAKA MPYA

WENGER AMEKUMBUKA KUCHEZA NA WEWE!


Huna haja ya kupeleka mawazo yako mbali. Itazame barcelona ya sasa na miaka miwili iliyopita. Bila shaka unapata picha ya Xavi,Iniesta,Messi na wenzao wakicheza soka ambalo siyo la kawaida duniani.

Misimu miwili iliyopita pale Camp Nou,hawa watu walitumia zaidi ya dakika 20 kwenye 'final third' ya Arsenal huku wakiandika mabao katika mchezo wa ligi ya mabingwa.
Kulikua na beki mmoja wa Arsenal anaitwa Michael Sylvestre,alipewa pasi kimakosa na Lionel Messi,Sylvestre akamrudishia Messi na akaenda kupiga bonge la goli.
Mtu mmoja akaniambia Barcelona hii inaweza kucheza hata bila kufumbua macho na ikashinda. Ni timu ya kuionea fahari hasa kwa Wahispania wenyewe kwa sababu asilimia kubwa ya wachezaji wao ni wazawa wa palepale Katalunya na hakuna mtu anatamani kuondoka pale.

Unawakumbuka watu hawa, Jens Lehman,Kolo Toure,Emmanuel Eboue,Robert Pires,Patrick Vieira,Gilberto Sylva,Jose Antonio Reyes,Thierry Henry,Dennis Bergkamp,Fredie Lgiumberg,Lauren Mayer,Sol Campbell,Ashley Cole,Edu,Ray Parlour,Sylvain Wiltord na Maritn Keown?

Hiki ndicho kizazi cha dhahabu cha arsenal. Achana na rekodi kilizoweka,lakini bado kilicheza soka lisilo la kawaida.Barcelona wanaweza kupigiana pasi fupi fupi lakini bado kuna kitu hawawezi kuifikia Arsenal ya kizazi hicho.

Sehemu ya kizazi hicho ndiyo iliyotandaza soka la uhakika pale Santiago Bernabeu.Arsenal hii ilikua haipigi tu pasi fupi fupi,la ilikua na mashuti ya Vieira,Chenga za Henry,kasi ya Reyes na magoli ya Bergkamp lakini bado mashabiki wa Uingereza walikua hawaionei fahari.walikua wanazipenda zaidi Man UTD na Liverpool. Unajua kwa nini?


Kulikua na Ryan Giggs na David Bekham pale Old Traford na Anfield kulikua na Michael Owen na Steven Gerald ambao wana asili ya England na walikua wakitamba.

Sol Campbell na Ashley Cole walikuwepo Arsenal lakini hakuwa waking'ara sana kama akina Bergkamp,Henry na Vieira (labda kutokana na nafasi zao). Waingereza hawakuongea sana kwa sababu timu ilikua inacheza vizuri sana.hivo Arsene Wenger aliwafunga midomo.


Arsenal ya sasa haipo vizuri sana kutokana na matatizo ambayo tulishayazungumza hapa kwenye 'the gunning machine'.Wadau wa sola la England wanaishutumu sana.Sasa kuna kitu cha maana Wenger amekifanya.Amewapa mikataba mirefu wachezaji watano wenye asili ya England.

Wachezaji hao wote wanapewa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Arsenal na kuna kila dalili kuwa baada ya muda watakua mastaa wa Arsenal.


Alex-Oxlade Chamberlain atacheza sana hata kama Teo Walcott atapewa mkataba mpya,
Kieran Gibbs tayari ana namba ya kudumu,
Carl Jenkinson anahitaji muda lakini atacheza pia kwa kua sioni kama Bacar Sagna ana maisha marefu pale.
Aaron Ramsey siyo kipenzi cha mashabiki lakini Arsene Wenger anafanya yote kuhakikisha anang'ara.
Jack Wilshere anang'ara sana kwa sasa na wadau wanamtaja kama nahodha ajaye wa Arsenal.

Unajua matokeo ya hiki anachokifanya Wenger?


Ramsey anacheza timu ya taifa ya Wales,hawa wengine wote watacheza timu ya taifa ya England. Watapendwa na Waingereza wote,vyombo vya habari vitawaandika vizuri na watapambwa sana.Watapewa bei kubwa kuliko thamani zao na watakua kama lulu. Hakuna atakayeisema vibaya Arsenal.ndivo waingereza walivo.

Na hivi arsenal hawamalizi katika nafasi mbaya kwenye EPL basi Wenger kwa hili amewaweza mashabiki na wadau wa soka la England.amecheza nao vizuri kama alivofanya Sir Alex Ferguson japo yeye alicheza karata tofauti.

Baada ya SAF kumkosa Mesut Ozil,akamkosa Wesley Sneijder,akamkosa Lucas Moura. Mashabiki wakaanza kumpigia kelele akaamua kucheza nao. Akamnunua mfungaji bora wa EPL msimu uliopita Robin Van Perse. Sasa hivi anafanya vizuri pale OT na hakuna anaekumbuka machungu ya kuwakosa Sneijnder,Ozil na Moura.


Hiyo ilikua karata sahihi.

Swali kubwa kwa Wenger ni kama hawa akina Wilshere,Jenkinson,Gibbs,Ramsey na Ox watafanya vizuri? Hatujui kwa sasa.

Imeandikwa na Richard Leonce ChardBoy
nipate ktk 0658399341 na chardboy77@yahoo.com kwa mawasiliano

3 comments:

  1. ngoja nikusaidie kidogo hawa wachezaji ulowataja hapa juu ni vijana wazuri ambao tunaamini kwa sasa wana perform vizuri kabisa no daut ila hawa hawataweza kukaa Arsenal ilo ndo tatizo kuna wachezaji wawili apo mali ya man united me nshawaona saa ivi tunamaliza tu kazi tuwachukue wengne watachukua wengne tatizo wenger ameshafanya arsenal ni chuo sio tena club yenye kuhitaji mafanikio

    ReplyDelete
  2. Unadhani Wenger anapaswa kufanya nini Bab?

    ReplyDelete

Powered by Blogger.