.........NAJUA WAJUA...........
VIWANJA 10 VIKUBWA ZAIDI KATIKA SOKA DUNIANI
Soka ni mchezo unaovutia zaidi mashabiki kuliko mchezo mwingine wowote duniani. Kutokana na hilo Viwanja vimezidi kuimarishwa ili kuweza kuingiza Watazamaji wengi zaidi na zaidi
Hapa tunawaletea viwanja 10 ambavyo vimeongoza kwa kuingiza watazamaji wengi zaidi waliokaa katika vitu.
Uwanja wa michezo mbalimbali lakini hasa Soka ulioko katika jiji la Pyöngyang Korea Kaskazini Ulifunguliwa Tarehe 1 May 1989( siku ya wafanyakazi) na una uwezo wa kuingiza watu 150,000 waliokaa.1. RUNGRADO MAY DAY STADIUM
Uwanja huu wa michezo mbalimbali na wenye uwezo wa kuingiza watu 120,000 Uko katika mji wa Bidhannagar, Kolkata, West Bengal nchini India.2. SALT LAKE STADIUM
Uwanja huu Umefunguliwa January 1984 na ni maarufu sana katika bara Asia hasa katika michezo ya Kriketi.
3. ESTADIO AZTECA
Uwanja huu Ulitumika katika michezo ya Olimpiki ya Summer 1968. Unauwezo wa kuingiza watazamaji 104,000, umejengwa katika jiji la Santa Ursula, Mexico City, Mexico na ni pia Uwanja wa Taifa wa Maxico kama Ulivyo uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Huu ni Uwanja wa Taifa wa nchi ya Malaysia wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 100,200 Ukijengwa kusini mwa mji mkuu wa Malaysia Kuala Lumpur.4. BUKIT JALIL STADIUM
Ni uwanja unaoweza kutumika katika michezo yote.
5. AZADI STADIUM
Zamani ulikua ukijulikana kama Aryamehr Stadium: Ni uwanja wa Taifa wa Iran uliopo katika Jiji la Tehran wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 100,000.
Uwanja huu Ulijengwa mwaka 1971 na kufanyiwa marekebisho makubwa mwaka 2003.
6: CAMP NOU STADIUM
Kwa Kiingereza unaitwa 'Nou Camp' wapenda soka wengi wanaujua huu kwani ni Uwanja unaotumiwa na Timu ya Barcelona ya Hispania Tangu mwaka 1957.
Uwanja huu uko katika kitongoji cha Catalonia,Barcelona Nchini Hispania.
Ukiwa na uwezo wa kuingiza watu 99,786.
7: FNB STADIUM (SOCCER CITY)
First national Bank Stadium ambao maarufu zaidi kama Soccer City au Calabash(kibuyu) umejengwa kwa msaada wa benki ya FNB mahali ambapo Raisi wa Kwanza Mwafrika wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela alitoa hotuba yake ya kwanza mara tu alipotolewa toka jela Mahali panaitwa Nasrec Soweto katika Jiji la Johannesburg karibu kabisa na yalipo makao makuu ya chama cha soka cha Afrika Kusini SAFA.
Uwanja huu unamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Johannesburg.
Ulijengwa wakati wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 ukiwa na uwezo wa kuingiza watazamaji 94,736.
Soka City ndo uwanja uliotumika kwa mechi ya Ufunguzi wa Kombe la Dunia mechi ambayo ni ya Kwanza ya Kombe la Dunia katika Ardhi ya Africa kati ya wenyeji Afrika Kusini dhidi ya Mexico na ndo uwanja ulimofanyika fainali ya kombe la Dunia kati ya Hispania na Uholanzi.
Inasemekana kuwa Wembley ndiyo uwanja ghali zaidi kuwahi kujengwa duniani. Ni uwanja wa Taifa wa England maarufu kama Uingereza. Uwanja huu upo Kaskazini magharibi mwa jiji la London. Uwanja wa Wembley una uwezo wa kuingiza watu 90,000 na hii ni baada ya kufanyiwa marekebisho mwaka 2006.8: WEMBLEY STADIUM
Uwanja huu hutumika kwa michezo mbali mbali mpaka mashindano ya magari
Hapa inaonekana pitch ya uwanja wa Wembley ikiwa imewekwa lami ili kufanyika mashindano ya magari
9: GELORA BUNG KARNO STADIUM
Uwanja wa taifa wa Indonesia Ukijengwa katika jiji la Senayan, Central Jakarta, Indonesia Ukipewa jina hilo kutokana na Rais wa Kwanza wa Indonesia Surkano.
Uwanja huu una uwezo wa kuingiza Mashabiki 88,000
Huu ni uwanja wa Jeshi la Misri ukiwa umejengwa magharibi karibu na bahari ya Mediterania10: BORG EL ARAB STADIUM
Uwanja huu umejengwa mwaka 2006 na una uwezo wa kubeba watazamaji 86,000
Tukutane mara nyingine katika NAJUA WAJUA nyingine
.....Edo Daniel Chibo....
Imetulia, nimeipenda
ReplyDeleteKuna haja ya kuupanua uwanja wetu ili nasi tuwe na cha kujivunia eh@ Abel
ReplyDelete