JULIO, ANATEMA MATE JUU KAMA SI KUNG'ATA KIDOLE CHAKE MWENYEWE


Nakurupuka kitandani asubuhi nikiwa sijui saa ngapi,naangalia kalenda ukutani nakuta ni Jumatatu, ooh siku mbaya sana inabidi niende shule, naangalia mishale ya saa yangu nakuta ni saa 12 alfajiri,sina haja ya kunyosha nguo zangu za shule, nlichokumbuka ni kupiga maji chap chap sikumbuki kama nilitumia sabuni,mzee wangu katulia varandani anaangalia BBC huku kijicho upande kikitazama movement zangu,huku akijipa moyo mtoto wake jinsi gani nnavyopenda shule, maana spidi ya kujiandaa haikuwa ya kawaida.
Kama kawaida nachukua buku(elfu moja) mezani,akaniongezea mia tano ya hamasa,maskini mzee., angejua nnachokiwaza kichwani asingenipa hata ile buku ya kwanza..
Nachukua zangu daladala kituo cha kushuka karume.. Naangalia saa yangu inaniambia saa 1 na robo na kipindi cha kwanza ni saa 1 na dakika 20,dakika tano zinatosha kabisa kunifikisha Benjamin Mkapa high school, nikiwa naelekea shule kulia naona geti limeandikwa kwa herufi kubwa TFF,Ooops hapa ndo nilipawaza kwanza pindi tu nilipoamka,ni mara chache sana nilienda shule moja kwa moja bila kupitia hapa..
Naingia ndani nakuta uwanja mtupu,lengo langu ni kuangalia mazoezi ya timu ya vijana (under 17), napiga moyo konde kuwasubiri nikiwa ndani ya senyenge huku wenzangu wakienjoy(wakifurahia) kipindi cha kwanza darasani,dakika kama 20 hvi mzee mmoja, rafiki yangu na mchezaji wa zamani wa Yanga na Castal union John Memba,akawa anaingiza mabench sehemu ya ndani ya uwanja.
Hapo nikapata uhakika wa kuwepo kwa mazoezi, sijakaa sana nikaona gari la kubwa lilobeba wachezaji,bila shaka hao walikuwa walengwa. Kabla mazoezi hayajaanza nilikua nimekaa kwenye benchi la ufundi,ungeniona ungefikiri ni kocha mtoto kama si mchezaji,wenye bench lao walivyoingia nikawapisha.
Nikatandika begi langu chini na kuligeuza kama kiti kisha nikaanza kuangalia mazoezi, nilipokua nimeketi haikua mbali na bench la ufundi.
Kipindi hiko ulikua mwaka 2006,vijana hao walikua wanajiandaa na mechi muhmu sikumbuki na nani.. Kuna wachezaji kama saba hawakua wageni machoni mwangu,Abeid kisiga(mdogo wake Shabani Kisiga) na Sabebe walikua wachezaj wa Rogastian Kaijage niliokua nawapenda sana.
Sijakaa sawa Kuna mtu kwenye benchi la ufundi akapiga simu kuelekea kwa mtu mmoja wa mpira anayeishi mwanza,ambaye mtoto wake ni mchezaji mashuhuri "ebwana eh mtoto wako ana miaka mingapi" akajibiwa "basi sisi tutapunguza mitano acheze kwenye timu yetu ya Taifa ya vijana" na walikua vijana wengi sana kati yao ambao wamezidi miaka 17. maskini Kaijage sikua na kifaa chochote cha kurekodi maneno hayo, nikabaki nahuzunika peke yangu. Ohh dhambi hii mpaka lini? Nikajiulza huku bench lao likiwa limeignore uwepo wangu,waliniona kama katoto kumbe nilikua nina akili ya kutambua wizi wanaofanya..
 Ama kweli mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu kama wiki mbili zilizopita kocha Julio alikua analalamika wachezaji wa Congo wamezidi umri miaka 17,eti anataka wapimwe tena anao uhakika wamezidi umri..
Huyu Julio anatema mate juu hajui kwamba yatamrudia mwenyewe.. Sio kwamba nakataa ila wachezaji wa bara letu wengi wao ni weredi wa kudanganya umri. Ila si tunapoamkia ndo wenzetu wamelalia.
Wachezaji wa timu ya vijana wa congo
 
                           
kocha julio
Timu ya vijana ya congo
                                                                                           



Haya ni baadhi ya matokeo ya timu ya vijana ya congo .. tangu waliposhiriki world cup ya u-17.

2 comments:

  1. amini usiamini wachezaji wa sasa ivi wa tanzania wale wadogo wote ni umri wao halali baada ya kufanywa progress zote za fifa tanzania imeingia woga nna kuanza kuchukua vijana wadogo sana, kipindi kile ulikosa nafasi kwa kuwa tu julio hakukujua na hamna mtu alokupeleka anaefahamiana na julio watanzania tuna umimina ubinafsi hasa linapokuja swala la nafasi ya kutoka kimaisha

    ReplyDelete
    Replies
    1. bab chiko who told u? kuna wachezaj kibao wanacheza under 17 ya sasa ni above 20 years old

      Delete

Powered by Blogger.