David Moyes ndio chaguo la Ferguson

David Moyes
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali David Moyes ndiye ambae anaonekana kuwa chaguo la kwanza la Sir Alex Ferguson pale Old Trafford pindi atakapostaafu, huku vyanzo hivyo vikieleza kwamba Mskotishi huyo anaamini kwamba bosi wa sasa wa Real Madrid Jose Mourinho anatakiwa kupewa kipaumbele zaidi ya Pep Guardiola kwa ajili ya nafasi hiyo kama itahitajika kufanya hivyo.

Meneja wa zamani wa Barcelona Guardiola amekuwa akihusishwa na Mashetani hao wekundu juu ya uwezekano wa kurithi mikoba ya Ferguson pale atakapostaafu. Na kwa mujibu wa gazeti la The Daily Express, inaaminika wawili hao watakutana mwishoni mwa juma kwenye jimbo la New York nchini Marekani.

Fergie ambaye anategemea kutimiza umri wa miaka 71 mwishoni mwa mwezi huu, inaarifiwa kwamba amemwambia kiongozi muandamizi wa klabu hiyo David Gill na wamiliki wa klabu hiyo Glazers kwamba, bosi wa sasa wa klabu ya Everton David Moyes ndie chaguo lake la kwanza kurithi mikoba yake.
Japokuwa Meneja huyo mwenye historia ya pekee kwa United anapendezwa na Guardiola, ila anaamini Moyes ni rafiki wa karibu ambaye ana uwezo wa hujenga uelewano mzuri wa matakwa ya soka la Uingereza na Primia Ligi kwa ujumla.

Chanzo kimoja cha karibu cha wachezaji wakongwe wa klabu hiyo kililitarifu gazeti la Daily Express.
 “Wanazungumzia juu ya Manchester kumchagua Guardiola kuwa mrithi wa Fergie”
“Mwenyewe Fergie ana machaguo yake makuu mawili David Moyes na Jose Mourinho.”
Chanzo hicho kiliongeza pia “Moyes  na Fergie ni watu walio karibu, na Fergie hupendezwa kwa namna vile ambavyo Moyes huwa anamuumiza kichwa pindi timu zao zinapokutana na hata pale anapokutana na timu nyingine kwa kipindi sasa”.

“Fergie anavutiwa pia na Jose ila kuna vitu vya msingi anavyoviona, kubwa ni juu ya tabia ya Mourinho ya kucheza na vyombo vya habari, kitu ambacho kitaweza kumfanya awe juu zaidi ya klabu.”

Ferguson mwenye mafanikio ya juu kama Meneja wa United, amefanikiwa kushinda mataji 12 kati ya 19 ya Ligi kuu ya Uingereza ambayo timu hiyo imeyapata mpaka sasa, huku akifanikiwa kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiriwa kwa muda mrefu na timu ya Liverpool ya kutwaa kombe hilo mara 18 mnamo mwaka 2011.


No comments

Powered by Blogger.