REKODI YA MAGOLI 100 YAWEKWA NA MAN UNITED KATIKA UWANJA WA LIVERPOOL
Jioni nzuri kwa mashabiki wa Manchester United duniani baada ya kushuhudia timu yao ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Liverpool katika dimba la Anfield.
Man United wakiwa katika kiwango kisichoridhisha ilijikuta ikipigana na kuzuia kabisa mashambulizi ya Liverpool ambao walikua katika hali nzuri kimchezo na kupata bao pekee katika dakika ya 78 likifungwa na Nahodha wake Wayne Rooney kwa shuti kali baada ya mpira wa kichwa uliopigwa na Fellain kugonga mwamba na kumrudia mfungaji.
Katika mchezo huo Man United ilipiga shuti moja tu golini kwa Liverpool shuti ambalo lilizaa goli hilo huku Liverpool wakishindwa kutumia vizuri mashuti yao 6 ambayo yaliokolewa vyema na David De Gea kipa wa United ambaye aliibuka kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Wayne Rooney amefikisha magoli 176 na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli mengi akiwa na klabu moja katika EPL
Liverpool ndiyo klabu iliyofungwa magoli mengi kwa mipira ya kona katika EPL ikiwa imefungwa magoli 7 msimu huu.
Man United imefunga katika mashuti manne waliyopia golini katika mechi zote mbili dhidi ya Liverpool msimu huu.
Kocha Van Gaal ameshinda mechi zote nne alizocheza dhidi ya Liverpool.
Man United wakiwa katika kiwango kisichoridhisha ilijikuta ikipigana na kuzuia kabisa mashambulizi ya Liverpool ambao walikua katika hali nzuri kimchezo na kupata bao pekee katika dakika ya 78 likifungwa na Nahodha wake Wayne Rooney kwa shuti kali baada ya mpira wa kichwa uliopigwa na Fellain kugonga mwamba na kumrudia mfungaji.
Katika mchezo huo Man United ilipiga shuti moja tu golini kwa Liverpool shuti ambalo lilizaa goli hilo huku Liverpool wakishindwa kutumia vizuri mashuti yao 6 ambayo yaliokolewa vyema na David De Gea kipa wa United ambaye aliibuka kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
MAMBO UNAYOPASWA KUYAFAHAMU BAADA YA MECHI HIYO
Manchester United Imefunga bao la 100 katika uwanja wa Anfield tangu timu hizo zilipoanza kukutana.Wayne Rooney amefikisha magoli 176 na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli mengi akiwa na klabu moja katika EPL

No comments