ZIDANE BAO 10 MECHI MBILI REAL MADRID IKIIPIGA SPORTING GIJON 5-1
Zinedine Zidane amefikisha mechi yake ya pili kama kocha mkuu wa kikosi cha Real Madrid kwa kuichapa Sporting Gijon bao 5-1.
Mchezo huo wa ligi kuu nchini Spain ulipigwa katika dimba la Santiago Bernabeu jijini Madrid nchini Spain ulikuwa nu wa pili kwa kocha mpya wa timu hiyo Zinedine Zidane baada ya kuibuka na ushindi mwingine wa bao 5-0 katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Deportivo La Coruña.
Cristiano Ronaldo na Karim Benzema walifunga goli mbili kila mmoja huku Gareth Bale akifunga bao moja na kufanya mchezo huo kumalizika kwa ushindi mnono kwa Madrid huku Gijon wakipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Isma Lopez.

UNAYOPASWA KUYAFAHAMU BAADA YA MECHI HIYO
- Karim Benzema alikua akiichezea Real Madrid kwa mara ya 300 tangu ajiunge nayo.
- Katika magoli 24 yaliyopita katika ligi ambayo Real Madrid wamefunga Ronaldo, Bale na Benzema wamefunga 23, Ronaldo akifunga (6), Gareth Bale (9) na Karim Benzema (8)
- Real Madrid wamefunga magoli 10 katika mechi mbili za kocha Zinedine
- Real Madrid wamefunga magoli manne ndani ya dakika 18 za Mwanzo hii ni mara ya kwanza kwa Real Madrid kufanya hivyo katika mechi za La Liga tangu mwaka 1956.
No comments