DANNY SSERUNKUMA APELEKA RAHA MSIMBAZI NA MAJONZI RUVU.


Baada ya kipigo toka kwa Mbeya City katikati ya wiki Simba leo ilirudi uwanja wa Taifa na kuwapa raha mashabiki wake baada ya kuibamiza JKT Ruvu Bao 2-1.


Alikua mshambuliaji Raia wa Uganda Danny Sserunkuma ambaye aligunga magoli yote mawili peke yake na kurudisha furaha kwa mashabiki wa Simba ambao walionekana kukata tamaa na timu yao baada ya kufungwa na Mbeya City Jumatano wiki hii.

Sserunkuma alitangulia kufunga bao kipindi cha kwanza kufatia kazi nzuri iliyofanywa na Emmanuel Okwi aliyeichambua beki ya Ruvu na kutoa pasi kwa mfungaji ambaye alifunga huku akizingirwa na beki wa JKT Ruvu.

JKT Ruvu walisawazisha kupitia kwa George Minja aliyetumia makosa ya kipa wa Simba Ivo Mapunda aliyetoka kuokoa mpira wa kona ya Haruna Shamte na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko wakiwa sare bao 1-1.

Okwi alimtengenezea Sserunkuma na bila ajizi Sserunkuma alifunga bao la pili likiwa ni bao lake la 3 katika ligi tangu ajiunge na Simba.
Mpaka mwisho wa mchezo Simba 2-1 JKT Ruvu simba wakipanda kipointi na kufikisha pointi 16.

No comments

Powered by Blogger.