MAN UNITED,LIVERPOOL NA SPURS ZATOA VIPIGO ENGLAND


Manchester United, Liverpool na Tottenham zote zimeibuka na ushindi katika mechi zao za leo katika mwendelezo wa Ligi kuu ya England jioni ya leo.

OLD TRAFFORD : MAN UNITED 3-1 LEICESTER CITY


Katika dimba la Old Trafford jijini Manchester mabingwa wa Historia wa ligi kuu ya England Man United waliibamiza klabu ya Leiceater City kwa jumla ya bao 3-1.

Kama ilivyokua katika pambano la awali pale katika dimba la King Power ndivyo ilivyokua leo kwa Man United kupata magoli matatu yote kipindi cha kwanza na kufanya kwenda mapumziko United wakiongoza kwa bao 3-0.

Robin Van Perse alitangulia kufunga akimalizia pasi ya Daley Blind kabla ya Radamel Falcao hajafunga bao la pili akiwa katikati ya msitu wa mabeki wa City.

Goli la 3 la Man United lilipatikana baada ya mpira wa kona iliyopigwa na nahodha Wayne Rooney kutua katika kichwa cha Beki wa Leicester City Wes Morgan na kujifunga alipotaka kuokoa.

Bao la kufutia machozi la Leicester Lilifungwa na Marcin Wasilewski akimalizia pasi ya Marc Albrighton dakika ya 80 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa ushindi kwa Man United wa bao 3-1.


ANFIELD : LIVERPOOL 2-0 WEST HAM

Mashabiki wa Liverpool leo walikua na vitu viwili vya kufurahia kwanza ikiwa ni ushindi kwa timu yao na pili kurudi uwanjani kwa mshambuliaji Daniel Staradge aliyekua majeruhi kwa muda mrefu.

Liverpool iliendeleza wimbi lake la Ushindi katika ligi kuu baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-0 wakiifunga timu ngumu ya West Ham.

Magoli ya Liverpool yalifungwa na Raheem Sterling dakika ya 50 akimalizia pasi ya Philippe Couinho kabla ya Daniel Sturadge hajafunga goli dakika 12 tangu alipoingia uwanjani akichukua nafasi ya Lazar Markovic pasi ya goli hilo ikipigwa na Philippe Countinho.

THE HAWTHORNS : WEST BROM 0-3 SPURS


Kikosi cha kocha Mauricio Pochettinho kikiwa Ugenini kiliweza kuivurumusha West Brom mabao matatu kwa Bila.

Shukrani zimwendee mshambuliaji Harry Kane aliyefunga mabao mawili peke yake huku lingine likifungwa kwa ufundi mkubwa na Christian Ericksen na kuwafanya Spurs kufikisha pointi 40 baada ya michezo 23 .

MATOKEO YOTE YA MECHI ZA LEO

Hull City.           0-3 Newcastle United
Crystal Palace 0-1 Everton
Liverpool.         2-0 West Ham United
Man United.     3-1 Leicester City
Stoke City.        3-1 QPR
Sunderland.      2-0 Burnley
West Brom.       0-3 Tottenham

~ Edo DC

No comments

Powered by Blogger.