YANGA YABUGIZWA 4 KWA WAARABU.

Wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki katika michuano ya kimataifa Yanga wamekumbana na kipigo cha bao 4-0 toka kwa Wenyeji USM Alger ya Algeria.

Mechi hiyo ya kwanza katika hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika CAF Ilishuhudiwa mpira wa upande mmoja zaidi wa USM Algeria baada ya Yanga kuonekana si lolote si chochote Kwa waarabu hao ambao walianza na kumaliza kwa kasi pambano hilo.

Iliwachukua dakika 4 tu USM ALGER kupata bao la kwanza lililofungwa na Darfalou baada ya makosa ya safu ya Ulinzi ya Yanga kisha Chafai akaiandikia timu hiyo ya ligi kuu ya Algeria bao la pili dakika ya 33 ambalo lilifanya matokeo kuwa 2-0 mpaka mapumziko.

Kipindi cha Pili USM Alger waliendelea kulishambulia lango la Yanga na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi yakifungwa na Meziane dakika ya 54 kisha dakika ya mwisho ya mchezo Wenyeji wakapata bao la 4 safari hii ni kwa njia ya penati iliyofungwa kiufundi na kipa wa timu hiyo Zemmamouche.


Matokeo hayo yanawafanya Yanga kushika mkia katika Kundi Lake huku USM  Alger wakiongoza wakiwa na pointi 3 zaidi wakati Rayon na Gormahia wote wana pointi Moja baada ya kutoka sare katika mechi ya mapema.

No comments

Powered by Blogger.