WANACHAMA SIMBA WARIDHIA MABADILIKO YA KATIBA

Wanachama wa Klabu ya Simba kwa kauli moja wameridhia na kupitisha mabadiliko ya katiba katika klabu ya Simba  kutoka umiliki wa wanachama na kwenda kwenye hisa kwa katika mkutano wa dharura uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Convention Center leo.
Mgeni Rasmi Dk Harrison Mwakyembe


Mgeni rasmi katika Mkutano huo alikuwa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe kabla ya kupitishwa kwa katiba alisema Serikali haijawahi kukataa mabadiliko kwa klabu yoyote isipokuwa imekuwa ikiagiza kufuatwa utaratibu wa sheria za nchi na katiba ya klabu husika hivpo kwa upande wa Serikali imeridhia kwa asilimia 100% mabadiliko hayo cha muhimu ni kuzingatia taratibu zote.


Mohammed Dewji 'MO' alishinda zabuni za kuwekeza ndani ya klabu ya Simba na ilikuwa inasubiriwa mabadiliko ya katiba ambayo yamekamilika huku mchakato mzima ukiendelea.

MO atawekeza hisa asilimia 49 zenye thamani ya shilingi bilioni 20 na kuifanya Simba kuendeshwa kisasa 




No comments

Powered by Blogger.