SIMBA YAENDELEA KUZIPIGA BAO YANGA, AZAM TUZO YA MCHEZAJI BORA VPL
Wekundu wa Msimbazi Simba wameendelea kuzitambia timu za Yanga na Azam FC baada ya kutoa idadi kubwa ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa 2017/18.
Tuzo hizo zitatolewa Juni 23 Katika ukumbi wa Mlimani City ambapo mbali na mchezaji bora kutakuwa tuzo ya kocha Bora, mchezaji bora kijana, tuzo ya heshima, goli Bora, Mwamuzi bora, Mwamuzi bora msaidizi na kikosi Bora cha Msimu.
Simba ambayo ametawazwa mabingwa wa michuano hiyo imetoa wachezaji saba kati ya 30 wanaowania tuzo hiyo wakati Yanga na Azam wakitoa watano kila mmoja.
Wachezaji wa Simba wanaowania tuzo hiyo ni nahodha John Bocco, Emmanuel Okwi, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Aishi Manula, Jonas Mkude na Shiza Kichuya.
Kwa upande wa Yanga wametoa wachezaji watano ambao ni Kelvin Yondani, Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajibu na Gadiel Michael Michael.
Azam wametoa wachezaji watano kwenye kinyang'anyiro hicho ambao ni Yahya Zayd, Razak Abalora, Agrey Morris, Himid Mao na Bruce Kangwa.
Singida United imetoa wachezaji watatu ambao ni Mudathir Yahaya, Shafiq Batambuze na Tafadzwa Kutinyu wakati Mtibwa ikitoa wawili ambao ni Hassan Dilunga na Shaban Nditi.
Wengine waliongia kinyang'anyiro hicho ni Adam Salamba (Lipuli), Habib Kiyombo (Mbao), Marcel Bonaventure (Majimaji), Mohamed Rashid (Prisons), Eliud Ambokile (Mbeya City) Awesu Awesu (Mwadui) na Khamis Mcha (Ruvu Shooting).

No comments