REAL MADRID YATANGULIA FAINALI MABINGWA ULAYA. 



Mabingwa watetezi wa michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya Real Madrid wametinga katika fainali ya msimu huu katika michuano hiyo baada ya sare ya bao 2-2 nyumbani dhidi ya Bayern Munich.

Ushindi wa bao 2-1 walioupata katika mechi ya awali Kule Ujerumani ulikua msaada Tosha Kwa Real Madrid ambao wametinga katika fainali yao ya tatu mfululizo kwenye michuano hiyo mikubwa katika ngazi ya klabu barani Ulaya.

Alikua Mshambuliaji Karim Benzema ambaye aliifungia Real Madrid mabao yote mawili la kwanza likiwa ni la kusawazisha baada ya Joshua Kimmich kutangulia kuipatia Bayern Munich bao la Kuongoza.

Mpaka Mapumziko timu hizo zilikua sare ya bao 1-1 na dakika chache baada ya kuanza kipindi cha pili makosa ya safu ya Ulinzi ya Bayern Munich yalipelekea Benzema kuiongezea Real Madrid bao la pili lakini James Rodriguez ambaye anaichezea Bayern Munich kwa mkopo aliisawazishia Bayern bao hilo na kufanya matokeo kuwa sare ya bao 2-2.

Licha ya kucheza vyema Bayern Munich walionekana kukosa mbinu za kuipita safu ya Ulinzi ya Real Madrid iliyokua ikiongozwa na Nahodha Sergio Ramos.

Matokeo hayo yanaifanya Madrid kutinga katika fainali za michuano hiyo Kwa ushindi wa jumla wa bao 4-3 na itasubiri mshindi Kati ya As Roma na Liverpool ambao wanacheza katika mechi ya marudiano na fainali mwaka huu zitafanyika katika jiji la Kyiy nchini Ukraine.

No comments

Powered by Blogger.