MAN UNITED YADUNDWA NA BRIGHTON UGENINI
Msimu wa ligi kuu ya England unakaribia kumalizika huku Klabu ya Manchester United Ikiwa imeweka historia mbaya zaidi baada ya kushuhudia Kwa Mara ya kwanza msimu huu ikifungwa na timu zote zilizopanda daraja na hii ni baada ya kukubali kichapo cha Saba msimu huu cha bao 1-0 dhidi ya Brighton.
Newcastle United, Huddersfied Town pamoja na Brighton zote zimepanda daraja na zote zimeweza kuibuka na ushindi katika mechi zao za nyumbani dhidi ya United huku Brighton ikishinda Kwa Mara ya pili dhidi ya United katika historia ya klabu hiyo Mara ya mwisho Ikiwa ni mwaka 1992.
Goli pekee la dakika ya 57 la mshambuliaji Pascal Gros ndilo lililoizamisha Manchester United licha ya juhudi za kuokoa mpira uliopigwa na Gros zilizofanywa na Marcos Rojo lakini Kwa msaada wa teknolojia ya goli mwamuzi aliweza kuruhusu mpira huo kuwa goli.
Ushindi huo unaifanya Brighton kufikisha pointi 40 katika nafasi ya 11 na kuihakikishia kubaki katika ligi kuu kwa msimu ujao huku Man United ikibaki na pointi zake 77 katika nafasi ya pili.
No comments