HATIMAYE YANGA YAFUFUKIA KWA MBAO
Wawakilishi waliobaki katika michuano ya kimataifa Yanga leo wameweza kupata ushindi wa kwanza baada ya michezo tisa kushindwa kupata ushindi wowote wakiifunga Mbao FC Kwa bao 1-0.
Mchezo huo pekee wa ligi kuu Soka Tanzania bara ulichezwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam umewarejesha Yanga katika nafasi ya kumaliza wakiwa katika nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi 51 katika nafasi ya tatu huku wakibakiwa na mechi mbili
Mfungaji pekee wa bao la Yanga Leo alikuwa ni Kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe Thaban Kamusoko dakika ya 25 ya mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wachache mno.
Baada ya mchezo huo Mfungaji wa bao la Yanga Thabani Kamusoko alilalamikia kubanana Kwa Ratiba ya mechi zao hali inayowapa ugumu wachezaji kupumzika wakiwa wametoka Shinyanga Jumamosi baada ya mchezo wao dhidi ya Mwadui na Leo Jumanne wakatakiwa kucheza tena na Mbao FC
Ushindi wa Leo pengine utaamsha ari ya ushindi Kwa mabingwa hao wa msimu uliopita wa ligi kuu Soka Tanzania bara baada ya kusota mechi 9 bila ushindi.

![]() |
Yusuph Mhilu akimtoka mchezaji wa Mbao Fc |

No comments