TFF YATAJA VIINGILIO MECHI YA SIMBA NA YANGA
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara(VPL) msimu wa 2017/2018 kati ya Simba na Yanga utakaochezwa Uwanja wa
Taifa Dar es Salaam.
Katika mchezo huo namba utakaofanyika saa 10
jioni Kiingilio cha chini kitakuwa shilingi Elfu Saba(7,000) wakati kiingilio
cha juu kitakuwa shilingi Elfu Thelathini.
Jukwaa la VIP A itakuwa shilingi Elfu Thelathini
(30,000),VIP B na C shilingi Elfu Ishirini (20,000) na Upande wa Mzunguko
kwenye viti vya rangi ya Chungwa,Bluu na Kijani itakuwa shilingi Elfu Saba
(7,000)
Viingilio
vimetangazwa mapema wiki mbili kabla ili kuwapa nafasi mashabiki wengi kununua
tiketi ili kuepuka usumbufu siku zikibaki chache.
Tiketi tayari zimeanza kupatikana kuanzia sasa
kupitia Selcom

No comments