SIMBA HAITANII AISEE, YAZOA POINTI 3 ZINGINE KWA MTIBWA
Vinara wa ligi kuu Soka Tanzania bara wekundu wa Msimbazi Simba wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kutoka Manungu mkoani Morogoro.
Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ulitawaliwa na ushindani mkali Kwa timu zote mbili huku Simba ikionekana kuwa makini zaidi kutoruhusu bao Kwa dakika zote 90.
Emmanuel Okwi ndiye aliyepeleka msiba Kwa Mtibwa na furaha Msimbazi akifunga bao pekee kipindi cha kwanza akitumia vyema mpira wa John Bocco bao ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.
Kwa matokeo hayo Simba inafikisha pointi 52 katika nafasi ya kwanza Ikiwa ni pointi 6 mbele ya Yanga wanaoshika nafasi ya pili ambao Jumatano hii watacheza dhidi ya Singida United.

No comments