RUFAA YA WAMBURA YAGONGA MWAMBA TFF
Kamati ya Maadili ya Rufaa ya Shirikisho la mpira wa
miguu Tanzania (TFF) imetupilia mbali Rufaa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa
Shirikisho la mpira wa Miguu Ndugu Michael Richard Wambura ya kufungiwa maisha
kujihusisha na soka.
Akisoma hukumu rufani hiyo Mwenyekiti wa kamati ya
Rufaa ya Maadili ya TFF, Wakili Ebenezer Mshana amesema Mawakili wa mrufani
walishindwa kujibu hoja za mteja wao, kufanya hivyo na kamati yake imeridhia
hukumu iliyotolewa na Kamati ya Maadili na kumtaka Wambura kuendelea na adhabu
ya kufungiwa maisha kujihusisha na soka.
Wambura alihumiwa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho
hilo mapema mwezi machi kutojihusisha na
soka maisha kwa makosa matatu.
(i)
kupokea pesa za malipo yasio halali
kinyume na sheria
(ii)
Kughushi barua ya kampuni ya JEKC ili
kulipwa isivyo halali
(iii)
Kufanya vitendo vilivyovunja hadhi ya
TFF.
"Hoja zote tatu alizotuhumiwa hakuna sehemu
yoyote kwenye ushaidi wao ambayo walikanusha kutenda kosa hilo, hivyo kamati imeridhia
bila shaka na hukumu iliyotolewa awali na Kamati ya nidhamu," alisem
Mshana.
No comments