REFA ALIKUA SAHIHI KUWAPA REAL MADRID PENATI ~ GRAHAM POLL
Aliyewahi kuwa mwamuzi bora kabisa kuwa kutokea nchini England Graham Poll ametanabaisha kwamba maamuzi ya jana usiku ya Refa Michael Oliver kuwazawadia Real madrid penati dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza na kumpa kadi nyekundu nahodha wa Juventus Gianluigi Buffon yalikua sahihi.
Real Madrid walitinga hatua ya Nusu fainali baada ya Kufungwa bao 3-1 dhid ya Juventus bao moja hilo la Madrid ambalo liliwapeleka Nusu fainali ndilo lililozua utata kwa mashabiki na watazamaji katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu
Mpira wa kichwa uliopigwa na Cristiano Ronaldo Ulimkuta Lucas vasquez akiwa katika eneo zuri la kufunga lakini beki wa Juventus Medhi Benatia aliyekua katika harakati za kuokoa kutoka nyuma ya Vazquez alionekana kumsukuma kwa nyuma Vazquez na mwamuzi Michae Oliver toka England akaamuru iwe penati na ndipo kulipotokea purukushani ya wachezaji wa juventus kumzonga mwamuzi hali iliyopelekea nahodha wao ambaye ni kipa namba moja wa timu hiyo Gigi Buffon kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Graham Poll ambaye huchambua matukio mbalimbali yanayotokea kwa waamuzi katika soka ameandika katika makala yake kwenye mtandao wa Daily mail kwamba maamuzi ya jana yalikua sahihi na anamsifia refa Michael oliver kwa maamuzi hayo magumu na ushujaa aliouonyesha wakati akitoa maamuzi yaliyolalamikiwa sana na Juventus na akasema alikua sahihi kabisa kwamba Benatia alimsukuma Vasquez.
NINI MAONI YAKO?
ANDIKA COMMENT HAPA CHINI
No comments