MZEE AKILIMALI: SIMBA HAIJATUZIDI CHOCHOTE ZAIDI YA LILE BAO
Katibu wa baraza la wazee wa klabu ya Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amesema watani wao wa jadi Simba hawakuzidi chochote zaidi ya bao walilofunga tofauti na ilivyotarajiwa.
Mzee Akilimali amesema Simba ilikuwa ikipewa nafasi ya kuifunga Yanga mabao mengi lakini ilikuwa tofauti na mechi ikawa ngumu kwa timu zote.
Katibu huyo aliwamwagia sifa wachezaji wake kwa kucheza soka na kuweza kuwadhibiti Simba ingawa hawakuwa na bahati ya kupata bao.
"Kitu pekee ambacho Simba ilituzidi jana ni lile bao, lakini vitu vingine tulikuwa sawa walicheza nasi pia tulicheza na mechi ilikuwa nzuri.
"Nilitegemea kuona kikosi cha bilioni moja kikitufunga sisi wenye matatizo mabao mengi lakini wamepata moja tena kwa bahati tu," alisema Mzee Akilimali.
Ushindi wa jana wa Simba umeifanya kuzidi Yanga pointi 14 lakini ina mechi mbili mkononi.

No comments