KLOOP AWAONYA NYOTA WAKE MECHI YA MARUDIANO YA ROMA
Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amewaonya
wachezaji wake kutobweteka na ushindi wa mabao 5-2 iliyopata jana dhidi ya AS
Roma katika nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kwakua miamba hiyo ya Italia
inaweza kupindua matokeo kwenye mechi ya marudiano.
Mjerumani huyo amewasisitiza wachezaji wake kuwa
mchezo huo bado haujamalizika wanatakiwa kuhakikisha wanashinda kwenye mechi ya
marudiano.
Kloop amesema amejifunza kitu kikubwa katika mchezo
huo kuwa wanaweza kushinda jijini Roma ingawa wapinzani wao wataingia kwa kasi
ya kutafuta mabao.
"Sisi sio Barcelona wenzetu wako bora ni
miongoni mwa timu tatu bora duniani, wameshinda mataji mengi lakini tutaenda
Roma kutafuta ushindi kwa hali yoyote ingawa itakuwa mechi ngumu kwa upande
wetu," alisema Klopp.
Katika mchezo wa kwanza wa robo fainali Roma
ilikubali kipigo cha mabao 4-1 kabla ya kuibuka na ushindi wa 3-0 kwenye mechi
ya marudiano kitu ambacho Klopp hataki kitokee.
No comments