GOLI 7 ZAFUNGWA MECHI YA LIVERPOOL NA ROMA UCL

Liverpool imeendeleza nia yake ya kutwaa taji la Ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu Kwa kuitandika As  Roma toka Italia bao 5-2 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliochezwa katika uwanja wa Anfield jijini Liverpool England.

Mchezaji bora wa mwaka wa Chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England Mohamed Salah ndiye aliyenogesha zaidi mechi hiyo akifunga mabao mawili na kutengeneza (Assist) Mara mbili katika ushindi huo mnono unaowafanya Liverpool kutanguliza mgumu mmoja ndani katika fainali ya michuano hiyo.

Roberto Firminho na Sadio Mane nao walifunga katika mechi hiyo, Firminho akifunga Mara mbili wakati Mane yeye licha ya kukosa magoli mengi lakini alifanikiwa kupata bao moja.

Edin Dzeko akifunga goli la kwanza la As Roma

Edwin Dzeko na Diego Peroti ndiyo waliwapa Roma Matumaini pengine ya kuweza kupindua matukeo katika mechi ya marudiano itakayofanyika jijini Roma Italia kila mmoja akisaidia kufunga bao moja na kufanya mchezo huo kumalika Kwa ushindi wa bao 5-2 walioupata Liverpool

No comments

Powered by Blogger.