YANGA YATUPWA NJE NA TOWNSHIP YAANGUKIA SHIRIKISHO
Wawakilishi wa
Tanzania katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika Yanga, wameondolewa
katika michuano hiyo leo baada ya sare ya 0-0 waliyoipata katika mchezo wao wa
marudiano dhidi ya Township Rollers ya Botwana katika mchezo uliochezwa katika
uwanja wa Gaborone huko Botswana.
Yanga wametolewa kwa
jumla ya mabao 2-1 ambayo yote yalipatikana katika mchezo wa kwanza uliopigwa
katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo haukua mwepesi
kwa Yanga ingawa walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwadhibiti washambuliaji
hatari wa Rollers ambao walikua wakiishambulia Yanga kwa muda mrefu lakini
walinzi wakiongozwa na Kelvin Yondani waliweza kuwadhibiti huku golikipa Youthe
Rostand akilazimika kuokoa mipira kadhaa ya hatari
Kwa matokeo hayo
sasa, Yanga wataangukia katika hatua ya mtoano ya kombe la shirikisho.
Yanga wao pamoja na
kujitahidi sana lakini walifanikiwakutengeneza nafasi moja pekee ya wazi katika
dakika ya 70 baada ya Pappy Tshishimbi kuupenyeza mpira uliomkuta Obrey Chirwa
katika nafasi nzuri lakini hata hivyo shuti la Chirwa halikulenga lango.
No comments